Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
mapema leo Agosti 11, 2017, imetangaza matokeo ya washindi wa shindano
la Afya na usafi wa Mazingira kwa mwaka 2017, iliyokuwa na kauli mbiu
‘Nipo Tayari’.
Akitangaza
washindi hao mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya, Jijini
Dar es Salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu amepongeza wadau mbalimbali kwa kuweza
kufanikisha zoezi hilo zikiwemo Halmashauri zote zilizoshiriki.
“Mashindano
ya afya na usafi wa mazingira kwa mwaka huu 2017 hapa nchini yaliweza
kushirikisha Halmashauri zote zaidi ya 185 huku, Halmashauri 73
zikishindanishwa Kitaifa baada ya mchujo ngazi ya Mkoa.
Mchanganuo wa Halmashauri hizi ni; Majiji Manne, Manispaa 21, Miji 21 na Halmashauri za Wilaya 27.
Kila
mwaka, Wizara yetu imekuwa ikiratibu mashindano haya Kitaifa nchini
kote ikiwa na lengo la kuinua hali ya afya na usafi wa mazingira katika
ngazi ya Kaya na taasisi ili kulinda na kuboresha afya ya jamii.”
Amesema Waziri Ummy Mwalimu.
Waziri
Ummy Mwalimu amewatangaza washindi wa kwa upande wa Halmashauri za
Majiji na Manispaa ambapo Manispaa ya Moshi ikiibuka kidedea kwa kupata
asilimia 78.5, mshindi wa Pili, Jiji la Arusha, Asilimia 78.1 na mshindi
wa tatu, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Asilimia 67.2.
Kwa
upande Halmashauri za Miji, mshindi wa kwanza ameibuka Halmashauri ya
Mji wa Njombe huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Halmashauri ya Mji wa
Kahama na mshindi wa tatu ni Halmashauri ya Mji wa Tunduma.
Washindi
wa Halmashauri bora inayotekeleza kwa ufanisi Kampeni hiyo hususani
katika ujenzi na matumizi ya vyoo bora, mshindi wa kwanza ni
Halmashauri ya Wilaya ya Meru, kwa mshindi wa Pii imechukuliwa na
Wilaya ya Njombe huku wa tatu ni Halmashauri ya Wilaya ya Makete.
Waziri
Ummy Mwalimu amewatangaza washindi wa Kijiji bora kinachotekeleza kwa
ufanisi hiyo ya usafi ni Kijiji cha Kanikelele kutoka Halmashauri ya
Wilaya ya Njombe, Mshindi wa pili, Kijiji cha Nambala kutoka Halmashauri
ya wilaya ya Meru, na cha tatu ni Kijiji cha Lyalalo kutoka Halmashauri
ya Wilaya ya Njombe.
Aidha
Vijiji hivyo viliweza kupatikana baada ya kushirikisha jumla ya Vijiji
na Mitaa 80 huku Kaya zake zikiwa zimefanikiwa kujenga na kutumia vyoo
bora pamoja na sehemu za kunawia mikono kwa maji na sabuni.
Washindi
wengine wa shindano hilo ni pamoja na Hospitali Bora kwa usafi ambapo
Mshindi wa kwanza ni Arusha Lutheran Medical Centre, mshindi wa pili,
Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Fransisco na Ifakara – Morogoro na wa
tatu, Hospitali ya Rufaa Mount Meru.
Aidha,
Waziri Ummy Mwalimu amewatangaza washindi kwa upande wa Hoteli, ambapo
Hyatt Regency Dar es Salaam the Kilimanjaro, iliibuka mshindi wa kwanza
huku wa pili ikienda Mount Meru Hotel, Arusha na ya tatu ni Aden
Palace Mwanza.
“Wizara
itatoa zawadi ya gari la kubebea taka (trekta lenye tela) kwa
Halmashauri ya Mji wa Njombe ambayo imeibuka mshindi wa kwanza kundi la
Miji.
Aidha
zawadi ya gari mpya aina ya Nissan itatolewa kwa Halmashauri ya Wilaya
ya Meru ambayo ilishika nafasi ya kwanza katika utekelezaji wa Kampeni
ya Taifa ya Usafi wa Mazingira, na zawadi za pikipiki aina ya YAMAHA kwa
washindi wote waliosalia ili kutoa motisha kwa mabwana Afya wote.
Pia
zawadi nyingine zitakazotolewa kwa washiriki katika makundi yote ni
pamoja Vikombe na Vyeti maalum ambapo Wizara tutaandaa siku maalum kwa
ajili ya kukabidhi zawadi hizo na tunawapongeza kwa ushindi” alimalizia
Waziri Ummy Mwalimu.
Katika
kuongeza ufanisi wa mashindano hayo, Wizara iliunda kamati maalum
ambayo iliratibu na kusimamia zoezi zima la uhakiki wa Mashindano huku
wajumbe wakitoka Taasisi mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Rais– TAMISEMI,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Maji na Umwagiliaji,
Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi – Muhimbili, Chuo Kikuu cha Ardhi, pamoja na wadau
wa Maendeleo wanaojihusisha na shughuli za Afya na usafi wa Mazingira
hapa nchini huku wakizingatia vigezo hali bora ya usafi wa mazingira kwa
ujumla.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
akizungumza na waandishi wa Habari katika mkutano wa tukio hilo Jijini
Dar es Salaam, la kutangaza washindi wa shindano la Afya na usafi wa
Mazingira kwa mwaka 2017, iliyokuwa na kauli mbiu ‘Nipo Tayari’.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
akizungumza na waandishi wa Habari katika mkutano wa tukio hilo Jijini
Dar es Salaam, la kutangaza washindi wa shindano la Afya na usafi wa
Mazingira kwa mwaka 2017, iliyokuwa na kauli mbiu ‘Nipo Tayari’. Kulia
kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Usafi wa Mazingira, Theophil
Likangaga.
Mratibu
wa kampeni ya mashindano hayo ya Usafi wa Afya ya Mazingira, Bw.
Anyitike Mwakitalima akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa tukio
hilo. Anayemfuatia ni Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalumu na kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma za Usafi wa Mazingira, Theophil Likangaga
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
akiwa na nembo ya kampeni ya NIPO TAYARI ambayo inahamasisha usafi wa
mazingira hasa usafi wa kunawa mikono na matumizi sahihi ya vyoo.
Mwanahabari wa mtandao wa Michuzi Media, Chalila Chibuda akiwa na nembo ya NIPO TAYARI
Mwanahabari wa Tumaini TV akiwa na nembo ya NIPO TAYARI
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
akiwa pamoja na baadhi ya wadau wa Wizara ya Afya katika habari na nembo
hiyo ya NIPO TAYARI
Mratibu wa kampeni ya mashindano hayo ya Usafi wa Afya ya Mazingira, Bw. Anyitike Mwakitalima akiwa na nembo ya NIPO TAYARI
Wadau mbalimbali wakiwa wamebeba nembo ya NIPO TAYARI
Wadau
mbalimbali wakivalishwa nembo maalum ya NIPO TAYARI kwa ajili ya
kuhamasisha Afya ya Mazingira ikiwemo usafi wa mikono na vyoo bora vya
kisasa
Wadau
mbalimbali wakivalishwa nembo maalum ya NIPO TAYARI kwa ajili ya
kuhamasisha Afya ya Mazingira ikiwemo usafi wa mikono na vyoo bora vya
kisasa
Andrew Chale
Blogger
Personality | Journalist | Activist | Online Editor dewjiblog |
Comedian |Volunteer Red Cross | Sauti za Busara & ZIFF Festivals
2007 to present.
Email: andrewchale@gmail.com
Phone: +255719076376 / +255767076376 / +255688076376
Telephone: +255222122830 Fax: +255222126833
Golden Jubilee Towers, Ohio Street,20th Floor
Po Box 20660, Dar es Salaam,Tanzania
EmoticonEmoticon