Wagombea sita wa Urais TFF uso kwa uso kwenye kipindi maalum leo Ijumaa saa 3 usiku, mbashara ndani ya TBC 1 na TSN online.

August 10, 2017
KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na Shirika la Utangazaji nchini (TBC) kesho Ijumaa (Agosti 11, 2017)wameandaa kipindi maalum kwa wagombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kitakachofanyika mjini Dodoma kuanzia majira ya saa 3 usiku.

Kipindi hicho maalumu kitarushwa mubashara kupitia TBC pamoja na ‘TSN Online’ kitawakutanisha wagombea urais; Ally Mayay, Fredrick Mwakalebela, Wallece Karia, Shija Richard, Iman Madega na Emmanuel Kimbe ikiwa ni saa chache kabla ya siku ya uchaguzi yaani kesho kutwa Jumamosi.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya kipindi hicho, Enock Bwigane alisema kuwa ili mpira wa miguu uendelee kukua nchini TBC na TSN iliona ni vyema ikawakutanisha wagombea kwenye jukwaa moja ili waweze kuwaambia wananchi ni kwa njia gani wataweza kuinua soka la Tanzania kama wakipewa dhamana hiyo.

Alisema, “Kuna takribani wapiga kura 130, wagombea urais ni sita lakini mmoja ndiye atakayeshinda na kuongoza shirikisho hilo kwa miaka minne kabla ya uchaguzi mwingine hivyo tumeona haja ya kuwakutanisha na kuwawezesha wananchi waweze kuwafahamu...

“…Naamini fursa ya kuwakutanisha na kuwapa nafasi ya kuwaeleza watanzania sera na mipango yao ya kuboresha soka ni jambo la msingi na ni haki yao ukizingatia kuwa leo ndiyo siku ya mwisho ya kampeni,” alisema Bwigane.

Naye Katibu wa kamati hiyo, Alfred Lasteck alisema kuwa TSN ikishirikiana na TBC inatambua nini watanzania wanataka kufahamu kuhusu mpira wa miguu na ndiyo maana imepanga kuwakutanisha wagombea ili waweze kuzungumza na umma kabla ya uchaguzi hapo kesho.

 “Kuna zaidi ya Watanzania milioni 50 ambao wangependa kufahamu ni nini kitasaidia soka la Tanzania ili liweze kuendelea kutoka lilipo sasa hadi kufikia mafanikio.

“Hivyo ni nafasi ya kipekee kwa kila mtanzania kufuatilia matangazo mubashara yatakayorushwa na TBC1 pamoja na TSN Online kipindi kile ambacho wagombea wote wa Urais watakapokuwa wakielezea mipango yao kuhusu mpira wa miguu nchini,” alisema Lasteck.
………..


Kwa mawasiliano zaidi;
0712046748
Alfred Lasteck


--

Mroki Mroki

C.E.O MD Digital Company & FK Blog

General Secretary PPAT

Professional Photojournalist & BLOGGER

P.O.BOX 110097,



Blog:  www.mrokim.blogspot.com   

DAR ES SALAAM, TANZANIA

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »