Mashindano ya Kigwangalla Cup 2017 yazinduliwa jimbo la Nzega vijijini

July 28, 2017
Mashindano ya mpira wa miguu kwa timu za Kata zilizo ndani ya Jimbo la Nzega Vijijini maalufu kama ‘Kigwangalla Cup’ yamezinduliwa rasmi jioni ya Julai 27, 2017 huku miamba 20 ikitarajiwa kuumana kumpata bingwa wa Jimbo hilo kwa mwaka huu.
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla aliwataka wachezaji wote wanaoshiriki michuano hiyo kuwa na nidhamu iliwaitumie michuano hiyo kama kipimo cha wao cha kuonesha vipaji vyao ili waonekane ngazi za juu.
“Mpambane kweli kweli. Kila mmoja wenu aoneshe uwezo wake wa kusakata kabumbu. Pia muzingatie nidhamu ya hali ya juu kwani michezo inaleta umoja na amani, inaimalisha afya ya miili yetu” alieleza Dk. Kigwangalla wakati akuzungumza na wachezaji katika ufunguzi wa michuano hiyo.
Dk. Kigwangalla pia alipata wasaha wa kukagua timu zilizofungua rasmi michuano hiyo kati ya Mizibaziba dhidi ya Nkiniziwa ambazo hata hivyo mpaka kipyenga cha mwisho zilitoka droo ya bao 1-1.
Dk. Kigwangalla alieleza kuwa, jumla ya Kata 19 za jimbo lake hilo zimeweza kutoa timu ilikushiriki michuano hiyo huku timu maalum ikiingizwa ambayo itajumuisha Madiwani wote kutoka Kata hizo ili kufanya jumla ya timu 20.
Dk. Kigwangalla alizitaja baadhi ya Kata zinazochuana kwenye michuano hiyo ni pamoja na Kata ya Puge, Ndala, Nata, Sanzu,Lusu, Milambo Itobo, Magengati,Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi.
Kata zingine ni Kata za Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe na Mwakanshanhala.
Awali kabla ya kuanza rasmi kwa mchezo wa ufunguzi, Madiwani wa Kata zote waliweza kukabidhiwa baadhi ya vifaa kwa timu zao sambamba na hilo wananchi waliweza kufurahia michezo mbalimbali ikiwemo ile ya jadi hasa mchezo wa asili wa bao la Kinyamwezi, kucheza drafti, kukimbiza kuku, michezo ya mbio kwa Wazee huku mchezo wa mbio kwa watu wenye vitambi ukitia fola kwenye ufunguzi huo, uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Nkiniziwa iliyopo kwenye Kata hiyo ya Nkiniziwa.
 
Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na timu ya Kata ya Mzibaziba wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.
 
Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wachezaji wa Kata ya Nkiniziwa wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.
Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wachezaji wa timu za Kata za Nkiniziwa na Mzibaziba wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.
Mtanange baina ya Mzimaziba dhidi ya Nkiniziwa ukiendelea katika mchezo wa ufunguzi wa Kigwangalla Cup 2017
Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu za Nkiniziwa na Mzibaziba (Msibasiba) wakati wa ufunguzi huo.

Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wananchi waliojitokeza kwenye tukio hilo la ufunguzi wa Kigwangalla Cup 2017
Wazee wakicheza mchezo wa bao la asili la kabila la Wanyamwezi wakati wa sherehe za uzinduzi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017
 
Timu zikichuana mchezo wa drafti
Wazee wakishindana katika kuwania kukimbiza Kuku
  
Hatmaye kuku alinyakuliwa na mshindi 
Mashindano ya kukumbia mita 100
Timu ya Wazee Nzega Vijijini wakipata picha ya pamoja
timu ya Madiwani wa Jimbo la Nzega Vijijini wakiwa kwenye picha ya pamoja
  
Mtanange huo ukiendelea kati ya timu ya Madiwani wa Jimbo la Nzega Vijijini na Wazee wa Nzega Vijijini
 
Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwapongeza Madiwani wa Jimbo laNzega Vijijini mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa kirafiki ambapo timu ya Madiwani waliibuka kwa ushindi mnono wa bao 1-0.
Wachezaji wa timu ya Mzibaziba (kushoto) pamoja na timu ya Nkiniziwa (kulia) wakiingia uwanjani wakati wa mchezo huo maalum wa ufunguzi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017.












--

Andrew Chale

Blogger Personality | Journalist | Activist | Online Editor dewjiblog | Comedian |Volunteer Red Cross | Sauti za Busara & ZIFF Festivals 2007 to present.


Telephone: +255222122830 Fax: +255222126833
Golden Jubilee Towers, Ohio Street,20th Floor
Po Box 20660, Dar es Salaam,Tanzania

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »