- Mkuu wa Masoko na Utalii, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Ibrahim Mussa akiwasilisha mada leo kwa wahariri na wanahabari waandamizi (hawapo pichani) kwenye semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kufanyika jijini Tanga.
- Mratibu Miradi wa Taifa, kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Gerald Kamwenda akiwasilisha mada leo kwa wahariri na wanahabari waandamizi (hawapo pichani) kwenye semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kufanyika jijini Tanga.
- Mratibu Miradi wa Taifa, kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Gerald Kamwenda akiwasilisha mada leo kwa wahariri na wanahabari waandamizi (hawapo pichani) kwenye semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kufanyika jijini Tanga.
- Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Magembe alipokuwa akizungumza na Wahariri na Wanahabari waandamizi (hawapo pichani) kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika semina ya mwaka 2017 iliyoandaliwa na TANAPA kwa wanatasinia hiyo ya habari.
- Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, ambayo ni wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, The African na Bingwa, Absalom Kibanda (kushoto) akiuliza swali kwenye semina hiyo. Wengine ni baadhi ya washiriki wa semina hiyo kwa wahariri na wanahabari waandamizi.
Na Joachim Mushi, Tanga
WAZIRI wa
Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Magembe amewaonya wananchi walio
jirani na hifadhi za taifa kuacha mara moja kitendo cha kuchanganya
mifungo na wanyamapori kwani kitendo hicho ni hatari kubwa kwa afya za
wananchi na mifugo yao. Alisema wanyamapori wana magonjwa mbalimbali na
hatari kwa afya zetu hivyo kitendo cha kuchanganya mifugo na wanyamapori
huamisha magonjwa kutoka huko na kuingia kwa wananchi wanapokula nyama.
Waziri
huyo mwenye dhamana na Maliasili na Utalii alitoa onyo hilo jana jijini
Mbea alipokuwa akifungua Mkutano na Semina ya mwaka kwa wahariri na
wanahabari waandamizi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa
(TANAPA). Alisema kitendo cha wafugaji kuchanganya wanyamapori na mifugo
ni changamoto nyingine kubwa, hivyo kuwaomba waandishi wa habari
kupitia vyombo vyao kutoa elimu kwa wafugaji. Alisema wanyamapori huwa
na magonjwa mengine ambao kwao hayana madhara makubwa lakini yanapoingia
kwa mwanadamu huhatarisha maisha yake kiafya.
"...Wananchi
kuingiza mifugo yao mbugani hili ni tatizo kubwa, tunaomba
mtusaidie...kwanza sheria zetu haziruhusu kabisa suala hili.
Tusichanganye mifugo na wanyamapori hii ni hatari tunaweza kubeba
magonjwa kule na yakawa na madhara makubwa kwetu...kuna magonjwa kama
kimeta, TB na homa za vipindi ambazo zipo kwa wanyamapori zikija kwetu
hizi ni hatari," alisisitiza Profesa Magembe.
Hata
hivyo, Waziri Magembe alipongeza juhudi zinazofanywa na wanahabari
kupitia vyombo vyao kwani wamekuwa msaada mkubwa kutoa elimu ndani na
nje ya nchi. Aliongeza kuwa matokeo ya wanahabari kutumia kalamu zao
kutangaza utalii yanajionesha wazi kwa ongezeko la idadi ya watalii
kutoka nchi mbalimbali kutembelea hifadhi zetu.
Aidha
ameitaka TANAPA kuendelea kushirikiana na wanahabari kwa kufanya semina
hizo kila mwaka ili kupata mrejesho juu ya kazi wanayoifanya, kwani
vyombo vya habari ni fursa nzuri ya kutoa elimu kwa umma na kutangaza
shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo. Mkutano huo wa siku
tatu ulioanza leo Julai 26 unatarajia kumalizika Julai 29, ambapo
wanahabari watajifunza na kujadiliana masuala mbalimbali ya utalii na
uhifadhi.
Idadi
kubwa ya watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani bado wanamiminika
kuja nchini Tanzania kutembelea vivutio anuai vya utalii. Alisema hali
hiyo imebainika baada ya ziara aliyoifanya kutembelea hoteli mbalimbali
za kitalii na kujionea namna zinavyopokea watalii mfululizo, huku baadhi
zikiwa zimejaa na wateja kulazimika kuweka oda mapema kabla ya kuanza
safari ya utalii.
"...Mimi
nimetembelea kabla ya kuja hapa baadhi ya hoteli kwenye maeneo ya
utalii kujionea, kweli hoteli baadhi zinawatalii wa kutosha kiasi kwamba
zingine zimejaa...mteja ukienda bila ya kufanya 'booking' ya chumba
huwezi kupata, hawana nafasi pia. Na watalii wanaokuja wanatoka kila
upande, kimsingi ujio huo wa watalii kwa wingi ni mafanikio yenu
wanahabari," alisema Waziri Prof. Magembe.
Alisema
watu wa kupongezwa ni waandishi wa habari ambao kiasi kikubwa;
ningekuwa na kofia hapa ningewavulia kwa heshima na kutambua mchango
wenu kwa kazi hii," alisema.
Hata
hivyo alisema bado suala la ujangili dhidi ya wanyamapori ni changamoto
japokuwa kwa sehemu kubwa kuna tunaweza kujivunia mapambano na jitihada
tulizozifanya kudhibiti hali hiyo. mabadiliko makndiyo wanaotumia
kalamu zao kuutangazia utalii wetu.
- sehemu ya washiriki wa Semina ya Wahariri na Wanahabari waandamizi kwa mwaka 2017 iliyoandaliwa na TANAPA.
- sehemu ya washiriki wa Semina ya Wahariri na Wanahabari waandamizi kwa mwaka 2017 iliyoandaliwa na TANAPA. Imeandaliwa;- www.thehabari.com
______________________________ ______________________________ _______________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
EmoticonEmoticon