Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sportpesa, Tarimba Abbas akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, ambapo alitoa shukrani kwa wanahabari, vyombo vya dola, serikali na watanzania kwa kufanikisha ziara ya timu ya Everton ya Uingereza hapa nchini. PICHA , HABARI NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Tarimba alisema kuwa ziara ya Everton nchini imekuwa ni ya mafanikio makubwa kimichezo, kiuchumi, kijamii na hasa kuutangaza vilivyo utalii wa Tanzania Duniani.
Tarimba hakusita pia kuishukuru Ikulu kwa kuwapa sapoti kubwa kufanikisha ziara ya Everton hasa katika masuala ya kumpata mgeni rasmi, Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na kuruhusu vyombo vya dola kwa ajili ya usalama wa timu hiyo.
"Kwa niaba ya SportPesa ambao ndiyo wadhamini wakuu wa timu hiyo, tutakuwa wachoyo wa fadhila kama tutashindwa kuwashukuru wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine walituunga mkono katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya ziara hii yanafanikiwa." Alisema Tarimba na kuongeza kuwa...
Napenda Kumshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa baraka zake, lakini pia nipende kumshukuru Makamu wake Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa utayari wa kuwapokea wageni wetu ."
Alimshukuru pia Waziri wa Habari, Utamadjuni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwa niaba ya wizara hiyo kwa kuwa bega kwabega katika jukumu hilo hizo. Pia hakusita kutoa pole kwa waziri huyo kwa kufiwa na mkewe.
Tarimba akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya kampuni hiyo, Oysterbay Dar es Salaam.
Tarimba akifafanua jambo wakati wa mkutano huo na vyombo vya habari.
Wanahabari wakisilkiliza majibu ya maswali yao waliyomuuliza Tarimba
EmoticonEmoticon