Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu
Benjamin Mkapa akimkabidhi Hati za Umiliki wa nyumba 50 za Watumishi wa
Afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita.
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu
Benjamin Mkapa akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na
Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita kabla ya kukabidhi
Hati za umiliki wa nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa
na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa hiyo mitatu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mikoa ya
Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita
baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa kukabidhi nyumba
50 kwa wizara ya Afya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya
Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kukabidhi nyumba hizo 50
zitakazotumika katika Sekta ya Afya katika mikoa ya Kagera, Simiyu na
Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa
awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakati Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akihutubia
wananchi wa Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya
Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kumaliza ziara yake Chato mkoani Geita
ambapo alikabidhi nyumba 50 zitakazotumika katika sekta ya afya katika
mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mama Anna Mkapa.
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu
Benjamin Mkapa akiangalia hotuba yake kabla ya kuhutubia wananchi
mbalimbali katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili
katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
Kikundi cha ngoma za asili cha Chato kikitumbuiza katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
Balozi wa Japan hapa nchini
Masaharu Yoshida akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chato Shaaban Ntarambe
hati ya kituo cha kukamua Mafuta ya Alizeti (Double Refine)
kilichojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali ya Japan. PICHA
NA IKULU
EmoticonEmoticon