Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb.) akiongea na baadhi ya wananchi wa
mtaa wa Mivinjeni Buguruni Sukita leo Alipowatembelea kufuatia kero ya
utiririshwaji wa maji yanayosadikiwa kuwa na kemikali kutoka katika baadhi ya viwanda maji
yanayotumiwa na wakazi wa maeneo hayo kwa kumwagilia bustani za mboga mbonga. Kutoka
kulia kwake ni Naibu Meya wa wa Manispaa
ya Ilala Bw. Omary Kumbilamoto, Afisa Mazingira Ilala Bw. Adon Mapunda na
Diwani wa kata ya Buguruni Bw. Adam Fugane.
Bwana Jafari Chimgege mratibu wa Mazingira kutoka Baraza la
Taifa la usimamizi na Hifadhi ya mazingira NEMC kanda ya mashariki akitoa
maelezo kwa Naibu Waziri Mpina kuhusu Kiwanda cha ANBANGS kinachomilikiwa na
raia wa China
kivyokaidi kutoa faini ya shilingi milioni 25, iliyotozwa mwaka jana mwezi
November kutokana na uchafuzi wa mazingira.
Naibu Waziri Mpina Akiongea na Wanahabari katika Bonde
Buguruni Sukita jijini Dar es Salaam
alipofanya Ziara leo.
Katika picha mboga za majani aina ya giligilani iliyopandwa
katika eneo la mivinjeni Buguruni inayosadikiwa kumwagiwa maji yenye kemikali
yatokayo viwandani.
Katika picha kijana ambaye jina lake halikupatikana
akimwagilia maji yanayosadikiwa kuwa na kemikali mbogamboga aina ya majani ya
Maboga zinazochipua katika eneo la mtaa wa mivinjeni buguruni sukila, leo.
(Habari na Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC
limepewa siku saba kukagua na kujiridhisha na uzalishaji, management na
utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake kwa Kiwanda cha
ANBANGS kinachotengeneza mifuko aina ya viroba vinavyotumika kama vifungashio
vya saruji, sukari na aina nyingine ya nafaka, na kukifunga kwa kile
kinachodaiwa kukaidi maagizo ya serikali ya awamu ya tano ya kutokulipa faini
kwa uchafuzi wa mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina alitoa agizo hilo Leo
alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Buguruni baada ya kupata malalamiko
yaliyoibuliwa na wakazi wa mtaa wa sukita mivinjeni kupitia kituo cha ITV ambapo Naibu waziri Mpina alitembelea eneo hilo na kujionena namna
ambavyo kiwanda hicho kinavyoendelea kutiririsha maji machafu.
Akiwasilisha taarifa ya ukaguzi wa kiwanda hicho Bw. Jafari
Chimgege ambae ni Mratibu wa mazingira kutoka NEMC kanda ya Mashariki
alimueleza Naibu waziri Mpina, kuwa “Kama
unakumbuka Mhe. Waziri Tulikuja hapa mwaka jana Novemver na tukafanya ziara na
ukaguzi hapa na kila tukija hapa hawa wachina wanashindwa kuonyesha ushirikiano
na kusema kuwa wao hawajui lugha ya Kiswahili, tuliona makosa mengi na
tuliwatoza faini ya shilingi milioni 25, na ilitakiwa walipe ndani ya wiki
mbili, lakini Mhe. Hiyo Faini haikulipwa. Na bado wanaendelea na uchafuzi wa
mazingira pamoja na kukaidi agizo za serikali.” Alisisistiza Chimgege.
Pamoja na maelezo hayo ya Bw. Chimgege Naibu Waziri
alielekeza Baraza hilo kupitia documents
zote muhimu zinazohusu, kiwanda hicho ambacho awali hakikuwa na cheti ya
tathmini ya athari ya mazingira wala vibali ya aina yoyote ya kutirirsha maji
yaliyotibiwa na kuuganishwa na mfumo wa mji taka wa DAWASCO hali ambayo
ilimpelekea Mpina pamoja na hilo kuagiza wamiliki wa kiwanda hicho kufikishwa
mahakamani
Katika Ziara zake za
ukaguzi wa Mazingira na viwanda jijini Da es Salaam, Mpina amehadi
kuingia hatua ya kushirikiana na mamlaka husika kuchukua sampuli za maji
yanayopita katika bonde la mto msimbazi katika eneo la viwanda vya karibu na
mtaa wa sukita mivinjeni ili kuyafanyia vipimo na kijirisha kama yana madhara
kwa viumbe hai na mazingira hususani mboga mboga zinazomwagiliwa maji katika
maeneo.
EmoticonEmoticon