Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina akisikiliza jambo kutoka kwa mmoja wa wadau hayupo
pichani, katika kikao kilichohusisha wamiliki wa viwanda na wenye mashule
wanaotoa maji taka kwa wingi jijini Dar Es Salaam, kikao hicho Pia kilihusisha
mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Dar es Salaam Dawasco na wamiliki
wa miundombinu hiyo Dawasa, kulia n Mratibu wa baraza la Taifa la Hifadhi
na usimamizi wa mazingira NEMC Bw. Jafari Chimgege.
Sehemu ya wadau walioshiriki katika kikao kilichohusisha
wamiliki wa viwanda na wenye mashule wanaotoa maji taka kwa wingi jijini
Dar Es Salaam, kikao hicho Pia kilihusisha mamlaka ya maji safi na maji
taka jijini Dar es Salaam Dawasco na wamiliki wa miundombinu hiyo Dawasa.
Katika picha ni sehemu ya wadau walioshiriki katika kikao kilichohusisha
wamiliki wa viwanda na wenye mashule wanaotoa maji taka kwa wingi jijini
Dar Es Salaam, kikao hicho Pia kilihusisha mamlaka ya maji safi na maji
taka jijini Dar es Salaam Dawasco na wamiliki wa miundombinu hiyo Dawasa.
Na EVELYN MKOKOI-DSM
Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amesema Serikali imejipanga kuondoa kero za
upatikanaji wa vyeti vya tathmini ya athari ya mazingira kwani imeonekana kuwa
ni kero kwa wawekezaji wenye viwanda nchini kwa kile alichokieleza kuwa
upatikanaji huo umekuwa ni wa mlolongo wa munda mrefu, gharama kubwa na urasimu
uliokithiri.
Mpina ameyaongea hayo leo Ofisini kwake mtaa wa Luthuli jijini
Dar es salaam alipokuwa katika kikao cha pamoja kilichohusisha baadhi ya wadau wamiliki wa viwanda na wenye
mashule jijini Dare s salaam ambao wanazalisha maji taka kwa wingi, pamoja na
mamlaka ya maji safi na maji taka Jijini Dar es Salaam na Pwani DAWASCO na wamiliki
wa miundombinu ya maji safi na maji taka Dar es Salaam DAWASA.
Naibu Waziri Mpina aliwataka wamiliki hao wa viwanda wahakikishe hawatatirirrisha
maji kiholela na kuwa na mfumo wa kuyatibu maji taka kabla ya kuyaondosha.
“ Nasisitiza kuwepo kwa ushirikiano kati ya wawekezaji wenye
viwanda hivi na DAWASCO na kuweza kutengeneza mfumo wa utendaji katika suala la
uondoshwaji wa maji taka kwa pamoja na niupate ndani ya siku saba.” Alisema
Mpina.
“ Kwa wamiliki wa viwanda mliyopo hapa nimeshafanya ziara za
ukaguzi katika viwanda vyenu halikadhalika na kwa wamiliki wa mashule, nawapa
miezi mitatu kwa kila mmoja wenu kuacha kutitirisha maji taka katika mazingira,
kuyatibu na kuyaelekekeza katika mfumo wa maji taka wa DAWASCO.
Aidha Naibu Waziri Mpina aliongeza kwa kusema kuwa Serikali
ya awamu ya tano haitakuwa na uvumilivu katika suala zima la uchafuzi wa mazingira
hasa kwa wenye viwanda, na itawachukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na
kuvifunga kabisa viwanda vitakavyo kaidi maagizo ya serikali kwa kuchafua mazingia.
Akiwasilisha Mpango Mpya wa mradi mpya wa kunusuru uchafuzi
wa mazingira utokanao na maji taka katika jiji la Dar es Salaam, Meneja
utendani kutoka DAWSCO Bi. Modester Mushi, Ameeleza kuwa shirika hilo limepata
ufadhili wa dola Milioni 600 za marekani kutoka kwa wafadhili wa maendeleo
wa shirika la maendeleo la Denmark, Bank
ya Maeneleo ya Ufaransa na Bank ya dunia utakaohusisha ujenzi wa miundombinu ya
majitaka na uondoshwaji na uhifadhi wa majitaka jijini Dar Es Salaam na Pwani.
Kikao cha Leo cha Naibu waziri Mpina na wamiliki wa shule na
wenye viwanda vinavyotoa maji taka kwa wingi na DAWASCO pamoja na DAWASA ni hatua ya awali ya kukabiliana na uchafuzi
wa Mazingira utokanao na maji taka jijini Dsm na Pwani.
EmoticonEmoticon