Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin
William Mkapa Chato mkoani Geita. Rais Mstaafu Mkapa katika siku ya kesho
anatarajiwa kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa
na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato
mkoani Geita. Rais Mstaafu Mkapa katika siku ya kesho anatarajiwa
kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na
Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita.
Kushoto ni Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu
Yoshida mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita. Balozi huyo wa Japan
katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi mtambo wa kukamua Mafuta ya
Alizeti (Double Refine) uliojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa
Serikali ya Japan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin
William Mkapa Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwa na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William
Mkapa pamoja na wageni mbalimbali waliofika Chato kwa ajili ya shughuli
mbalimbali za kimaendeleo zinazotarajiwa kufanyika kesho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
mkoani Geita Josheph Kasheku Msukuma aliyefika Chato pamoja na Mkuu
wa Mkoa wa Geita. PICHA NA IKULU.
EmoticonEmoticon