Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akionyesha jambo kwa Mkuu wa Wilaya
ya Ilala, Sophia Mjema wakati wa ziara yake aliyoifanya mapema hii leo
jijini Dar es salaam ya kukagua uchafuzi wa mazingira katika Dampo la
Pugu Kinyamwezi lililopo Wilaya ya ILala.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira, Luhaga Mpina akizumgumza na waandishi wa habari mara baada
ya ziara hiyo aliyoifanya katika Dampo la Pugu Kinyamwezi lililopo Ilala
jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akibadiishana mawazo na Mkuu wa Wilaya
ya Ilala, Sophia Mjema(katikati), Sophia Mjema na kushoto ni Meya wa
jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita wakati wa ziara ya ukaguzi wa uchafuzi
wa mazingira uliofanyia katika dampo la Pugu KInyamwezi jijini Dar es
salaam.
NA EVELYN MKOKOI
Kufuatia ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina, iliyofanyika Jijini Dar es Salam leo katika Manispaa
ya ilala, iliyohusisha ukaguzi wa Dampo la Pugu Kinyamwezi, Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kupitia Mkaguzi wa Mazingira
wa kanda ya Mashariki Bw. Jaffari Chimgege imeitoza faini Manispaa
ya jiji ya Dar es Salaam kiasi cha shilingi Milioni 25.
Faini hiyo inatokana na kosa la
uchafuzi wa Mazingira wa kutohudumia Dampo hilo ipasavyo na kupelekea
harufu mbaya, vumbi na maji yenye sumu kali na kuhatarisha afya ya
wakazi wa maeneo jirani viumbe hai na mzingira kwa ujumla.
Kufuatia malalamiko ya wakazi wa mtaa wa Viwege uliyopo katika kata
ya Majoe yaliyowasilishwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bi Amina
Rashid yaliyoeleza kuwa na changamoto mbali mbali katika dampo hilo
zikiwemo za vumbi na maji yenye kemikali kwenda katika maeneo ya makazi.
Naibu Waziri Mpina, ameitaka Halmashauri ya jiji kuja na mpango mkakati
utakaoweza kuupunguzia mzigo dampo la Pugu ambalo kwa sasa linatumika
kupokea takataka zote za Halmashauri za jiji la Dar es Salaam na kuonekana
kulemewa na mpango huo uwezeshe kila manispaa kuwa na dampo lake.
Aidha Mpina alibaini kuwepo kwa madhaifu makubwa katika ukusanyaji
wa mapato yatokanayo na kuondosha taka katika manispaa za jiji na kuutaka
uongozi wa jiji Hususan Mkurugenzi wa Jiji kufuatilia madeni hayo kikamilifu.
Pamoja na kutoa deadline ya uwasilishwaji wa fedha hizo “ni vyema ghahama
za uondoshwaji wa taka zikatokana na taka zenyewe na siyo kutoa fedha
za kuhudumia taka kutoka katika vyanzo vingine vya mapato. Alisisitiza
Mpina.”
Mpina pia aliitaka manispaa ya jiji kutafuta namna bora ya kuondosha
taka sumu na kuelekeza taka zote za matairi katika jiji la Dar es Salaam
zitafutiwe sehemu tofauti na namna pekee ya kuzitekekeza.
Akionekana kuongea kwa hasira na msisitizo Naibu Waziri Mpina alisema, “ Hakuna kitu nisichopenda katika utendaji wangu kama kuona taasisi
za serikali zikiwa za kwanza katika suala zima la uchafuzi wa mazingira na
faini hiyo jiji mtailipa ndani ya siku 14 lakini pia kuhakikisha mnarekebisha
matobo yote yanayolalamikiwa kupitisha maji na kupeleka katika makazi
ya wananchi.
Lakini pia hilo litaendana pamoja na kujenga mifereji ya maji ya mvua, na maji ya sumu
yaende katika mkondo sahihi wa maji hatarishi na bila kusahau kuruhsu
maji hayo baada ya kujiridhisha na vipimo vinavyotakiwa.
Awali akitoa taarifa ya hali ya mazingira na usimamizi wa taka
katika Dampo la Pugu Kinyamwezi , Mkuu wa Idara ya usimamizi taka
wa jiji la hilo Bw. Shedrack Maximillian alimueleza Mpina kuwa jiji
linakabiliana na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja dampo kupata
moto, dampo kutokuwa la kisasa na maji yenye sumu kwenda katika makazi
ya wananchi.
Hata hivyo Manispaa ya ilala imetenga kiasi cha fedha shilingi Bilioni
moja za kitanzania kwa mwaka wa fedha ulioisha pamoja na kuzungumza
na wadau wa maendeleo ikiwa ni mkakati madhubuti wa kuweza kuboresha
Dampo hilo kinalotumika kwa kiasi kikubwa na manispaa zote za jiji la
Dar es Salaam.
EmoticonEmoticon