Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kupungua kwa bei za dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutokana na uamuzi wa serikali wa kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Viongozi wakiwa meza kuu kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Victoria Elangwa, Mkurugenzi Mkuu MSD, Laurian Bwanakunu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Kaimu Mfamasia Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya, Siana Mapunjo na Mfamasia kutoka Wizara hiyo, Mercy Masuki.
Taarifa ikitolewa.
Baadhi ya Wafanyakazi wa MSD wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanahabari Ibrahim Yamola akiuliza swali.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanahabari, Philip David akiuliza swali.
Picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema bei za dawa, vifaa tiba na Vitendanishi vya maabara zinazonunuliwa na kusambazwa Boahari ya Dawa (MSD) zimepungua bei kwa asilimia 15 hadi 80 ukulinganisha na mwaka jana kutokana na hatua ya MSD kuanza utaratibu wa kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kama alivyo agiza Rais Dk.John Magufuli.
Waziri huyo ameyasema hayo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, alioufanya ofisi za Makao Makuu ya Bohari ya Dawa MSD, Keko, Dar es Salaam leo huku akizielekeza Halmashauri, Hospitali na Vituo vya Afya kutumia bei elekezi ya dawa iliyotolewa ma Wizara ya Afya ambayo ipo kwenye kitabu ya orodha ya bei cha MSD.
MSD kwasasa inaagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wanchizipatazo 20 ambazonipamojana Kenya, Uganda, Afrika Kusini, India, Bangladesh, Pakistan, Jamuhuri ya Watu wa Korea, China, Ujerumani, Uingereza, Uswisi, Denmark, Ufaransa, Ubelgiji, Italia, Romania, Marekani, Cyprus, Falme za Kiarabu, na Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema tayari wametoa mikataba 73 kwa wazalishaji ambapo kati ya hiyo 46 ni ya wazalishaji wa dawa ambao wanatoka nchi za Uganda, Denmark, Ufaransa, Ujerumani, China, Afrika Kusini, Nchi za Falme za Kiarabu,Bangladesh, India, Kenya na Tanzania ambao wanazalishia aina 178 za dawa.
Baadhi ya dawa hizo ni pamoja na dawa ya chanjo ya homa ya ini (hepatitis B Vaccine ) awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 22,000 sasa inauzwa shilingi 5,300, Dawa ya sindano ya Diclofenac kwa ajili ya maumivu (vichupa 10) awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 2,000 sasa inauzwa shilingi 800 na Dawa ya kupambana na maambukizi ya bacteria (Amoxicillin/Clavulanic Acid Potassium 625mg) yenye Vidonge 15 awali iliuzwa shilingi 9,800 sasa inauzwa shilingi 4,000.
Kwa upande wa vifaa tiba amesema jumla ya wazalishaji 18 wamepata mikataba ambao wanatoka Uingereza, Ujerumani, India, Kenya na Tanzania, kwa ajili ya aina 195 za vifaa tiba.Aidha, kwa upande wa vitendanishi vya maabara, jumla ya wazalishaji 9 kutoka nchi za Uingereza, Ujerumani, Ubelgiji, Romania, China, India na Kenya wamepata mikataba kwa ajili ya aina 178 za vitendanishi vya maabara.
Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Serikali ya awamu ya tano imeboresha kwa kiasi kikubwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini ambapo bajeti ya dawa,vifaa tiba, vitendanishi vya maabara na chanjo kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018 ni shilingi Bilioni 269 kutoka Bilioni 251 ya mwaka jana wa fedha 92016/2017)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
EmoticonEmoticon