Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
nchini Marekani na Canada, Col. Aldoph Mutta (kushoto) akimlaki Balozi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson
Masilingi siku ya Jumamosi June 17, 2017 siku Mhe. Balozi alipokua
mgeni rasmi kwenye futari ya pamoja inayoandaliwa na Jumuiya ya Waislam
DMV (TAMCO) Silver Spring, Maryland.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico
Mhe. Wilson Masilingi akipokewa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam DMV
(TAMCO) ustaadh Ally Mohamed mara tu alipowasili na kujumuika na
wanajumuiya hao waislam wa DMV na marafiki zao katika futari ya pamoja
iliyofanyika siku ya Jumamosi June 17, 2017 Silver Spring, Maryland.
mwenyekiti wa TAMCO ustaadh Ally Mohamed akimwongoza Balozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson
Masilingi ndani ya ukumbi.
Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Col. Aldoph Mutta, mkuu wa idhaa
ya Kiswahili Voice of America (VOA) Dr. Hmza Mwamoyo, Balozi wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi
na The Maryland House of Delegates Legislative District 41 Baltimore
City Mhe. Bilal Ali ambaye nae alialikwa na Jumuiya hiyo kwenye futari
ya pamoja DMV.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico
Mhe. Wilson Masilingi na The Maryland House of Delegates Legislative
District 41 Baltimore City Mhe. Bilal Ali wakiongozwa na mkuu wa idhaa
ya Kiswahili Voice of America (VOA) Dr. Hmza Mwamoyo kwenye futari ya
pamoja iliyofanyika siku ya Jumamosi June 17, 2017 Silver Spring,
Maryland.
Kutoka kushoto ni Mke wa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico mama Marystela Masilingi, Balozi Liberata Mulamula, Zawadi Sakapala na dada Jasmine wakipata futari.
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
EmoticonEmoticon