NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA
la Umeme Nchini, (TANESCO), limewahakikishia watanzania kuwa mradi wa
umeme wa gesi wa Kinyerezi II unaendelea kwa kasi kubwa na utakamilika
kama ilivyopangwa.
Hakikisho
hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito E.
Mwinuka, wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa umeme wa gesi wa
Kinyerezi II jijini Dar es Salaam, ambao unatarajiwa kutoa Megawati 240
za umeme.
“Niwahakikishie
watanzania kuwa ifikapo Agosti mwakani (2018), mradi wa umeme Kinyerezi
II utakamilika na hivyo tutaongeza Megawati 240 kwenye gridi ya Taifa.”
Alisema Dkt. Mwinuka wakati akitoa majumuisho ya ziara yake.
Dkt.
Mwinuka alifuatana na wakurugenzi watendaji wasaidizi, Mhandisi
Abdallah O. Ikwasa, (anayeshughulikia Uzalishaji), Mhandisi Khalidi
James, (anayeshughulikia uwekezaji miradi) na Mhandisi Kahitwa Bishaija
(anayeshughulikia Usambazaji).
Dkt.
Mwinuka alisema watanzania wanahitaji umeme ulio wa uhakika na kwamba
Serikali kupitia TANESCO imejipanga kuhakikisha umeme wa uhakika
unapatikana kwa watanzania na hivyo kuchangia pato la taifa.
“Kama
mjuavyo serikali imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha Shirika
linatekeleza miradi hii na tayari shilingi Bilioni 110 zimetolewa na
serikali katika kutekeleza mradi huu wa Kinyerezi II.” Alifafanua Dkt.
Mwinuka.
Awali
Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Stephens S.A.Manda, alisema, wataanza
kuingiza umeme kwenye gridi ya taifa kila mwezi kuanzia Desemba mwaka
huu 2017 ambapo Megawati 30 zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa.
“Tuna
mashine 8 ambazo zitafua umeme huo kwa hiyo kuanzia Desemba Mosi mwaka
huu, tutaingiza megawati 30 kwenye gridi ya taifa na tutafanya hivyo
kila baada ya mwezi mmoja kwani tunaelewa kuwa serikali ambayo
imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda, tunaona umeme ni hitajio muhimu
kwa hivyo kila tutakapokamilisha mtambo mmoja tunaingiza umeme kwenye
gridi ya taifa hatutasubiri kuwasha mitambo yote minane.” Alisema
Mhandisi Manda.
Mhandisi
Manda alisema, mradi mzima ambao umeanza kutekelezwa rasmi Machi 3,
2016, utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 344,059,746.00 kati ya
hizo asilimia 15 zimetolewa na serikali.
“
Kufikia leo Juni 17, 2017, asilimia 63 ya ujenzi wa mitambo
imekamilika, na tunahakika ya kukamilisha ujenzi wa jumla kwa vile
tayari mitambo yote inayohitajika imeshalipiwa na mingine iko njiani
inaletwa nchini.” Alifafanua na kuongeza mitambo yote iliyoagizwa na
TANESCO imo kwenye makontena 900 na tayari makontena 400 na ushee
yamekwishawasili na baadhi ya mitambo imefungwa na tunatarajia mashine
zingine kwenye hayo makontena yaliyosalia zitawasili nchini wakati
wowote. Alisema.
Akizungumzia
kuhusu makontena 20 yaliyokuwa yamezuiliwa na TRA bandarini, Mhandisi
Manda alisema, taarifa hizo hazina msingi wowote kwani kiasi hicho cha
makontena 20 ni sehemu ya makontena 900 na tayari TANESCO imeshalipa
fedha hizo za kodi na mizigo hiyo imefika site.
Katika
ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Mwinuka ;pia
alitembelea mradi wa umeme wa upanuzi wa Kinyerezi II ambako nako
ameridhishwa na kasi ya ujenzi wake.
Mradi
huo ambao unasimamiwa na Mhandisi Simon Jilima, utawezesha ongezeko la
megawati 35 na hivyo Kinyerezin I ambayo inatoa Megawati 150 itakuwa na
uwezo wa kutoa Megawati 185 za umeme.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka (katikati),
akiongozana na Meneja wa mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, Mhandisi Simon
Jilima,(kushoto) na Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere,
wakitembelea kukagua maendeleao ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II na
ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, leo Juni 17, 2017.
Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda
DKT.
Mwinuka, (kulia), Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia
miradi, Mhandisi Khalid James, (katikati) na Meenja Mradi wa Kinyerezi
II, Mhandisi Stephen A.S.Manda, wakijadiliana jambo
Mitambo ikiteremshwa eneo la ujenzi
Mkurugenzi wa Business Times, Imma Mbuguni, (kulia) akizungumza jambo na Mhandisi, Khalid James
Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere(kulia), akiteta jambo na Kaimu Meneja Uhisano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji
Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme (Generation), Mhandisi Abdallah O.
Ikwasa(kulia), akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere
Mhariri Mtendaji wa Business Times, Bw. Imma Mbuguni, akizungumza ili kuoata ufafanuzi wa maswala kadhaa
Baadhi ya mitambo ikiwa eneo la ujenzi ikisubiri kuunganishwa
Mtandao wa nguzo za umeem ukiwa tayari kwa sehemu kubwa
Kaimu
Meenja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji akifafanua baadhi ya mambo
kuhusu namna Shirika hilo linavyotekeleza sera ya kusaidia jamii
(Corporate Social Responsibility), ambapo alisema, licha ya shirika
imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii sio tu kwenye maeneo ambako mradi
unapita bali pia maeneo mengine na kutolea mfano wa tetemeko la ardhi
Mkoani Kagera, kamati ya kikosi kazi cha kuokoa mazingira, na hata
shule. Kushoto ni Dkt. Mwinuka na Mhandisi Khalid James
Dkt. Mwinuka akiwa amezungukwa na wasidizi wake akizungumza kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II
Dkt. Mwinuka (kulia), akiongozana na wakandarasi toka kampuni ya kijapani SUMITOMO amabao ndio wanajenga mradi huo
Dkt. Mwinuka (kushoto), Mhandisi Ikwasa(katikati) na Mhandisi Chegere
EmoticonEmoticon