31 Mei, 2017
Jumla ya shilingi milioni 180
zimekusanywa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora katika kipindi cha Mwezi huo
kutokana na makosa mbalimbali yaliyofanywa na waindeshaji wa vyombo vya moto.
Takwimu hizo zilitolewa jana
mjini Tabora na Kamanda wa Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa wakati wa mkutano
na waandishi wa habari ofisi kwake wakati akitoa ufafanuzi juu ya jitihada
mbalimbali wanazozifanya katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu mkoani humo.
Alisema makusanyo hayo
yametokana tozo kwa madreva wa magari, pikipiki na bajaji na waendesha baiskeli
walivunjia Sheria za Usalama barabarani katika kipindi hicho.
Kamanda alitaja baadhi ya makosa
ni madereva wa Bodaboda kutovaa kofia ngumu wao na abiria wao , madereva wa
magari kuendesha bila kuwa na leseni, mwendokasi, kutozingatia alama za
barabara na kupakia abiria zaidi ya uwezo wa chombo cha usafiri.
Kamanda Mtafungwa alitoa wito
kwa watu wote wanaoendesha vyombo vya moto Mkoani Tabora kuepuka kuvunja Sheria
za Usalama Barabarani ili waokoe fedha wanazozipata zitumike kusaidia familia zao
katika matumizi mengine ya maendeleo
badala kulipa faini.
“Naomba waendeshaji wa vyombo
vya moto kuzingatia Sheria za Usalama barabarani ili wasipigwe faini ambazo
zinawafanya watoe fedha ambazo zingewesaidia wao na familia katika shughuli
mbalimbali” alisema Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora.
Aidha , alitoa wito kwa vijana
wote wanaoendesha Bodaboda na baiskeli maarufu kama daladala kujisajili katika
vituo(vijiwe) na kukaa katika maeneo yao waliopagwa na viongozi wao ili kuwasaidie
kuwafichua baadhi ya Wahalifu kujificha katika usafiri huo.
Kamanda Mtafungwa alisema kuwa
hatua hiyo itasaidia kuwabaini baadhi ya wahalifu ambao wanapenda kujificha
katika kazi hiyo kwa kutokubali kukaa eneo moja kwa hofu ya kubainika uovu wao.
Katika hatua nyingine Jeshi la
Polisi Mkoani Tabora linawashikilia watu sita wakiwemo madereva wa bodaboda
wawili kwa tuhuma za kuvunja nyumba usiku na kuiba na wengine kununua mali
inayodhaniwa ni ya wizi.
Kamanda Mtafungwa alisema kati
ya watuhumiwa hao wanne walikiri kuhusika na uvunjaji nyumba na kuiba mali na
wengine wawili walikutwa na mali zinazodhaniwa kuwa za wizi.
Aliwataja waliokamatwa kwa
tuhuma za kuvunja nyumba ni Issa Maganga(27), Salum Maganga(19), Hamis
Malale(24) na Amri Salum (20) wote wakazi wa Ipuli katika Manispaa ya Tabora .Kamanda Mtafungwa aliongeza
kuwa walikutwa na mali zinazodhaniwa kuwa za wizi ni kuwa nia Maganga Salum(28)
na Hussein Salum (28) wote wakazi wa Kiloleni Manispa ya Tabora.
Alivitaja vitu vilivyokamatwa
ni pamoja na tairi za baiskeli 21, mzani mmoja na mawe yake, mikasi saba ya
baiskeli , minyororo nane ya baiskeli, televisheni mbili inchi 32 , solar inchi
24 na kandambili jozi saba.
Vingine ni sigara pakiti 20 ,
Betri za radio jozi 18 , dawa za meno aina ya Whitedent na mafuta ya kujipaka.Alisema kuwa watuhumiwa hao
walishindwa kudhibitisha uhalali wa mali hizo na hivyo nao wanatarajiwa
kufikishwa Mahakamani wakajibu makosa yanayowakabili.
Kamanda huyo alitoa wito kwa
vijana mkoani Tabora kuacha kujiingiza katika vitendo vitakavyosababisha
kukamatwa na hatimaye kupelekwa Mahakamani na kuongeza kuwa ni vema wakashiriki
katika shughuli mbalimbali kama vile kilimo cha bustani ili kujipatia kipato
halali badala ya kufikia kuvunja nyumba na maduka ya watu wengine
EmoticonEmoticon