Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 akizungumza Na Watendaji wa
Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo,
Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es
salaam ametoa maelekezo 17 ya kuzingatia katika utendaji wao.
*1.*Watendaji wa Sekta ya Ardhi
Na Ujenzi Kushughulikia migogoro ya ardhi Na Ujenzi ili wananchi
wasipeleke malalamiko yao ngazi za juu.
*2.*Watendaji wa Sekta ya Ardhi
Na Ujenzi Wameagizwa kutoa vibali vya Ujenzi ndani ya mwezi mmoja Na
zoezi hilo lianze Mwezi wa sita mwaka huu 2017. Mwanzoni mwa mwezi wa
Saba kuzinduliwa teknolojia ambayo wananchi watapata taarifa zao za
Ardhi kwenye mtandao Jambo ambalo litafanya Dar es salaam kuwa kiganjani
mwa wananchi.
*3.*Wakuu wa Idara katika Sekta
ya Ardhi Na Ujenzi kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu Mipango ya Idara
kwenye vyombo vya habari kwa kuwatumia maafisa habari kwani tayari wana
mahusiano Na waandishi mbalimbali katika vyombo vyombo vya habari.
*4.*Wakuu wa Idara ya Ardhi Na
Ujenzi kutoa TAARIFA ya maeneo yote ya wazi yaliyotolewa Hati, Na
kujitokeza haraka kwa wote waliotoa Hati za maeneo ya wazi kama wapo.
*5.*Wakuu wa Idara ya Ardhi Na
Ujenzi kusimamia haraka upimaji wa maeneo yote ya Umma kama kama vile
Shule, Hospitali, Na Masoko kama alivyoagiza Waziri wa TAMISEMI sambamba
Na kutoa Mikakati wa Upimaji.
*6.*Wakuu wa Idara ya Ardhi Na
Ujenzi kuhakikisha ufanisi Na bidii ya utendaji inaongezeka hususani
mikakati ya kuhusisha wapimaji binafsi wanaotambulika kwani Mji ukipimwa
vyema Madiwani watafurahi lakini pia itakuwa njia rahisi ya kuepuka
migogoro ya Ardhi.
*7.*Kushughulikia changamoto za kisera unaofanya utaratibu wa Upimaji Na utoaji wa Hati kuchelewa kukamilka.
*8.*Mabaraza ya Kata kuangaliwa upya kwa mujibu wa Sheria ili kuwa Na utendaji imara unaoshabihiana Na Jambo la kisera.
*9.*Kila Mtumishi kufanya Kazi
yake kwa Uaminifu kwani dhamani aliyopewa ni kubwa Na anapaswa kuitendea
Haki. Watumishi wote kusimamia Na kutekeleza ilani ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kwani chama hicho ndicho kimeingia mkataba Na wananchi
katika kipindi cha miaka mitano.
*10.*Kila Mkuu wa Idara kupitia
ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015-2020 ili kutambua
maelekezo yaliyobainishwa katika Sekta yake sambamba Na kuwaelekeza
wasaidizi wao pia kuisoma Na kuielewa vyema ilani hiyo.
*11.*Kufatilia Na kufahamu
upandaji wa madaraja Na stahiki zao kwani ni Haki zao za msingi kisheria
ikiwa ni pamoja Na kwenda likizo.
*12.*Watumishi wote kuheshimu mamlaka walizonazo Na kutumia vikao halali kutoa taarifa sahihi kwa watu husika.
13. Kuwa Na ushirikiano wa watumishi katika Idara zote ili kukuza ufanisi wa Kazi.
*14.*Kujitokeza ndani ya wiki
moja kwa watumishi wote wa Sekta ya Ardhi waliojihusisha Na utoaji wa
Hati za Ardhi kinyume Na sheria. Na endapo wasipojitokeza Na wakabainika
watachukuliwa hatua za kisheria.
*15.*Kufafanua baadhi ya mambo
ili Madiwani waweze kuelewa. Sambamba Na kutoogopa maadhimio kama
wanatenda Kazi kwa mujibu wa Sheria pasipo kupendelea.
*16.*Wakuu wa Idara kila mwisho wa wiki kutoa taarifa kwa Wakurugenzi inayoonyesha idadi ya Migogoro Na jinsi ilivyotatuliwa.
17.*Katika kupunguza changamoto
ya kuwafikia wananchi kwa Wakati RC Makonda Amesema atatoa *Pikipiki 5
kwa kila manispaa ya jiji la Dar es salaam, yaani jumla ya pikipiki 25
kwa manispaa zote 5 za Sekta ya Ardhi kwa kila Manispaa.
Safi sana Rc Wetu Paul Makonda hii ndio CCM mpya kuelekea Tanzania Mpya.
Hapa kazi tu.