Mwanamuziki Naseeb Abdul aka
Diamond Plutnamz akiwasili kwenye maduka makubwa ya GSM Mall Barabara ya
Nyerere leo tayari kwa kuzindua Pafyum yake inayoitwa (CHIBU), Diamond
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo amesema
ameamua kuingia kwenye soko la kutengeneza pafyum zenye nembo yake CHIBU
ili kusaidia serikali katika suala zima la kutatua changamoto ya uhaba
wa ajira nchini.
Ameongeza kwamba kuanza
kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira kwa vijana wengi
lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi zitakazotozwa
kutokana na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake wote wanaweza
kuitumia, Pafyum ya CHIBU itapatikana katika maduka yote ya GSM na
itauzwa bei ya rejareja kiasi cha shilingi 105.000 kwa moja.
Katika mkakati mwingine wa soko
Meneja wa Msanii huyo Bw. Salaam Mendes amesema wako katika mazungumzo
na mashirika kadhaa likiwemo shirika la ndege la Kenya Airways kwa ajili
ya kuitangaza bidhaa hiyo na kuifikisha kwenye soko la kimataifa ikiwa
ni pamoja na kuuzwa katika maduka makubwa kwenye viwanja vya ndege
katika nchi mbalimbali ambako ndege za shirika hilo zinafika
Mwanamuziki Naseeb Abdul aka
Diamond Plutnamz akizungumza na waandishi wa habari wakati akizindua
Pafyum hiyo kulia ni Mmoja wa Mameneja wake Babu Tale.
Mmoja wa mameneja wa Diamond Plutnamz akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo.
Mwanamuziki Naseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akionyesha Pafyum ya CHIBU ambayo ndiyo kwanza imeingia sokoni.
Meneja wa Diamond Plutnamz Bw.
Salaam Medes akizungumza mara baada ya kuzindua pafyum hiyo kwenye duka
kubwa la GSM Mall barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Mwanamuziki Naseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akionyesha chupa ya pafyum ya CHIBU aliyoizindua leo jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki Naseeb Abdul aka
Diamond Plutnamz akimkabidhi chupa ya Pafyum Aisha Azori mteja wake wa
kwanza aliyenunua bidhaa hiyo kwenye maduka ya GSM Mall jijini Dae
salaam.
Bw. Salaam Mendes akitaja bei ya pafyum hiyo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuizindua rasmi leo jijini Dar es salaam.
EmoticonEmoticon