Muuza CD za Tamthilia na Filamu za nje,Marick Omary,akizungumza na waandishi wa habari katika Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuiomba serikali kuwasaidia na kutowafungia vijana hao kuuza cd hizo kwa kuwa zinawapatia ridhiki ya kihalali tofauti na kufanya kazi zingine zisizo za kihalali.
Muuza CD za Tamthilia na Filamu za nje,Andhuhuri Mohamedy,akichangia hoja kwa waandishi wa habari katika Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuiomba serikali kuwaruhusu wafanyabiashara hao (Machinga) kuendelea na biashara hizo ambayo inawawezesha kulisha na kusaidia familia zao na kusema kama kuna maboresho ni bora serikali wakae kwa pamoja wazungumze siyo kupiga marufuku watakufa njaa.
Muuza CD za Tamthilia na Filamu za nje,Halima Bakari,akizungumza kwa majonzi kuhusu kuiomba serikali kuweka utaratibu mzuri wa kuwaruhusu wafanyabiashara hao waendelee na uuzaji wa tamthilia na filamu za nje kuendelea kuuza kwa kuwa kuna wanawake wengi wameachana na suala la kuuza miili yao (Biashara ya Ngono) ambayo siyo halali wakajiingiza kuuza cd hizo ili wapate kipato cha kihalali kwa hiyo kuwafungia ni kuwarudisha nyuma kifikra.
Baadhi ya wauzaji wa CD hizo waliokusanyika katika eneo hilo la Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
Vijana ambao ni machinga wanaouza CD za Tamthilia na filamu za kizungu,Kihindi na za kutoka bara la asia wakionesha cd hizo juu wakati wa mkutano na waandishi wa habari mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
|
Imeandaliwa
na mtandao wa www.elisashunda.blogspot.com/E mail:elisashunda@gmail.com
/0719976633
NA ELISA SHUNDA,DAR
WAFANYABIASHARA wadogo wadogo ‘Machinga’
wanaouza filamu za kigeni wameandamana wakiomba kukutana na Rais John Magufuli
ili kusikilizwa juu ya kupigwa marufuku kuuza filamu hizo hapa nchini.
Marufuku hiyo ilitolewa na Waziri wa
Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Harrison Mwakyembe, siku chache baada ya
kuteuliwa katika nafasi hiyo mara baada ya kukutana na waigizaji wa ndani
ambapo walieleza malalamiko yao juu ya filamu za nje kuharibu soko la kazi zao.
Wamachinga hao waliandamana jijini
Dar es Salaam jana katika soko la Kariakoo katika Mtaa wa Aggrey ambako kuna maduka wanakoenda kuchukua mikanda ya
filamu za nje ‘CD’ na kusambaza mtaani huku wengine wakiweka katika vibanda kwa
ajili ya kukodishia wateja wanaohitaji.
Wakizungumza na waandishi wa habari
wafanyabiashara hao walisema Waziri huyo alitoa maamuzi hayo kwa kusikiliza
upande mmoja ambao ni walalamikaji bila kuwapa nafasi ya kujieleza jambo ambalo
wanalipinga.
Mmoja wa machinga hao Hanzuruni
Mohamed alisema aliyekuwa Waziri katika Wizara hiyo Nape Nnauye alikuwa
akisikiliza pande zote kabla kufanya maamuzi na kuongeza kwamba walishakaa
vikao mbalimbali kwa ajili kutafuta mwafaka lakini Mwakyembe ameshindwa kufanya
hivyo.
“Nape alikuwa anafanya maamuzi kwa
kufuata pande zote mbili, huyu katoa siku 10 tu kufungia filamu za nje, hapa
kuna vijana zaidi 1000 fikiria tutafanya kazi gani, tukiwa panya road nchi
itakuwaje tunakuomba Rais uliangalie hili sisi ni vijana wako” alisema Mohamed.
Naye Halima Bakari alisema kufungwa
kwa biashara hiyo kutamwathiri maisha yake kwani alikuwa akitegemea biashara ya
filamu kuendesha maisha yake na kuhudumia familia yake na kusema awali alikuwa
akifanya biashara ya kujiuza biashara aliyoiacha baada ya kujiingiza katika
soko la filamu.
“Mwanzo nilikuwa najiuza nategemewa
na mdogo wangu yatima, sasa hivi mabosi wamefunga maduka wakisema wanaogopa
kufungwa kutokana na kauli ya Waziri, sasa hivi hatuna ajira nyingine mimi ni
binti bila kutoa penzi sipati kazi na kauli mbiu ni Hapa kazi tu, Rais tusaidie
tutaenda wapi” alisema Bakari.
Kwa uapnde wake Maliky Ally alisema
wametii kuacha kuuza filamu lakini wamaomba kusikilizwa upya ili kuwe na
makubaliano yatakayohusisha pande zote kwasababu hiyo ni ajira wanaoitegemea
kuendesha maisha yao.
Imeandaliwa
na mtandao wa www.elisashunda.blogspot.com/E mail:elisashunda@gmail.com
/0719976633
EmoticonEmoticon