RAIS MAGUFULI ZITUPIE MACHO BANDARI BUBU

April 02, 2017
SERA ya RAIS Dkt John Magufuli ya Serikali ya Viwanda ni nzuri kwani ina lengo kubwa la kuhakikisha inarudisha Tanzania ya Viwanda ili kufungua fursa na kimaendeleo na kukuza uchumi.
 
Jitihada hizo zimeanza kuzaa matunda kwenye maeneo mbalimbali kutokana na kuanzishwa viwanda ambazo leo hii vimekuwa na faida kubwa kwa watanzania kwa kupata ajira ambazo zimewasaidia kukabiliana na ugumu wa maisha.

Lakini pia kusaidia wakulima ambao wamekuwa wakizalisha mazao
mbalimbali yatokanayo na matunda kupata soko la uhakika kutokana nauwepo wa viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali zinazotokana nauzalishaji wao.

Licha ya kuwepo kwa jitihada hizo za Serikali ya Viwanda lakini bila kuangaliwa kwa umakini maeneo ya usafirishwaji ikiwemo Bandari Bubu ambazo zimekuwa ni sehemu kubwa ya kuingiza na kusafirisha bidhaa mbalimbali bila kulipa kodi jambo ambalo linachangia kurudisha nyuma fursa ya kimaendeleo na kukuza uchumi wa nchi ikiwemo kupotea kwa mapato.
 
Hali hii imekuwa ikijitokeza kwenye mikoa mbalimbali ambayo
imezungukwa na ukanda wa bahari ya hindi na hata wakati mwengine maziwa kitendo ambacho kinachangia kukwamisha juhudi za serikali kukusanya ushuru ambao unaweza kuwasaidia harakati za kiuchumi.

Licha ya maeneo hayo kutumika na wafanyabiashara kwa kukwepa kulipa ushuru lakini hali hiyo pia inasababusha shehena ambazo zilikuwa zikipita kwenye Bandari mbalimbali kupungua kitendo ambacho ni hatari kwa ufanisi wao.
 
Kwa mkoa wa Tanga zipo Bandari Bubu zipatazo 45 ambazo zimekuwa zikifanya shughuli zao nyakati mbalimbali licha ya kufanya hivyo ni kinyume cha utaratibu uliowekwa na hivyo kuisababishia mamlaka husika kukosa mapato.
 
Bandari Bubu ambazo zimekuwa zikitumika kwa wingi kuingiza mizigo na bidhaa mbalimbali kwa njia za magendo zipo ambazo zimekuwa zikifanya kazi hizo ni Kigombe iliyopo wilayani Muheza,Kipumbwi iliyopo wilayani Pangani,Jasini wilayani Mkinga na Sahare iliyopo wilaya ya Tanga.

Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri Badari Bubu ya Sahare ni miongoni mwa eneo ambalo mwanzoni mwa mwaka huu kulitokea kazia ya Jahazi kuzama likiwa na bidhaa zilizodaiwa kuingizwa kimagendo mkoani hapa .
 
Jahazi hilo lilizama baada ya kupigwa na dhoruba kubwa ya mawimbi na hivyo kupoteza mwelekeo na kuzama licha ya kwamba nahodha wao kuwataka wenyewe mizigo kuipunguza.
 
Uwepo wa Bandari hizo kumechangia kwa asilimia kubwa upungufu wa shehena inayosafirishwa kupitia Bandari ya Tanga pamoja hali iliyosababisha kupungua uwezo wao kukusanya mapato .
Jambo hilo linapaswa kuangalia kwa umakini na mamlaka husika ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama ili kuweza kudhibiti hali hiyo kabla haijaleta athari kubwa kwa ukuaji na ustawi wa Bandari
Kwani jambo hilo limekuwa changamoto kubwa sana kwao kuweza kufikia malengo yao ambayo ni kuongeza wigo mpana wa ukusanyaji wa mapato ambayo yanaweza kusaidia kukuza kipato chao na Taifa kwa ujumla.

“Kama ni kikwazo kwa Bandari ya Tanga hili nalo lipo hivyo ni wajibu wa mamlaka husika kuakikisha wanalivalia njuga jambo hilo kwa mapana kusudi changamotohiyo iweza kuondoka”
 
Kwani ni dhahiri kubwa iwapo shehena inayosafirishwa kwa njia zisizo rasmi inasababisha kupotea kwa mapato ambayo yangeweza kuongeza kasi na ufanisi wa Bandari ya Tanga kutokana na kukusanya mapato.
 
“Kwa kweli uwepo wa Bandari zisizo rasmi hii umekuwa changamoto kubwa sana na imechangia hata upungufu wa shehena inayosafirishwa kupitia Bandarini na kama usipozibitiwa hali inaweza kuwa mbaya”
Katika jambo hilo lazima kuwepo kwa juhudi za makusudi kwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kuangalia namna ya kuzifuatilia kwa karibu uondoaji wa Bandari Bubu ambazo zimekuwa kikwazo cha maendeleo.

Lakini pia watu wanaotumia Bandari hizo kuachana na shughuli
hizo kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria za hapa nchini na kuwepo kwa adhabu kali kwa watakaobainika kujihusisha na suala hilo ili kuweza kulitokomeza la sivyo tutaendelea kuongeza kila siku bila majibu
 
Nimalizie kwa kumuomba Rais Magufuli atupie macho na uwepo wa Bandari hizo kwani nazo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa mamlaka za Bandari maeneo mengine kupungua kwa shehena za mizigo jambo linaathiri ukuaji na ustawi wake

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »