Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameunda kamati ya watu watano
kuchunguza suala la kilichotokea Clouds Media siku ya Alhamisi pamoja na
Ijumaa usiku.
Kamati hiyo imeundwa baada ya
Waziri Nape kufanya ziara Clouds Media leo Jumatatu 20/03/2017 na
kuzungumza na uongozi wa Clouds Media kufuatia tukio la Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam kutembelea ofisi hizo siku ya Ijumaa usiku akiwa na askari
wenye silaha.
Kamati hiyo itaongozwa na
Mwenyekiti Dkt. Hassan Abbas Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO, Bw.
Deodatusi Balile Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Ndg. Jesse Kwayu
Mhariri Mtendaji Gazeti la Nipashe, Ndg. Mengida Johannes kutoka Wapo
Redio pamoja Ndg. Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA).
Baada ya kamati hii kufanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha kutoka pande zote mbili Wizara itasema hatua itakazochukua.
Imetolewa na:
Zawadi Msalla
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
EmoticonEmoticon