CHAMA
Cha CCM Mkoa wa Kigoma kimevuna jumla ya Wanachama wapya 868 kutoka
vyama mbalimbali vya siasa akiwemo mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo
Venasi Busunzu wa wilaya ya Kakonko na Mwenyekiti wa CUF Kilembwe Omari
mgombea udiwani kata ya Sinuka wamekabidhiwa kadi ya chama hicho jana,
katika hitimisho ya sherehe za madhimisho ya kutimiza miaka 40 ya CCM.
Akihitimisha
sherehe hizo jana zilizo fanyika Kimkoa Katika kijiji cha Mwakizega
Wilayani Uvinza Mwenyekiti wa CCM kigoma Amani Kabourou , alisema katika
maazimisho waliyafanya Mkoa mzima katika Wilaya zote walipatikana
wanachama wapya 726 na kutoka vyama vya upinzani ni wanachama 146 ambao
walikabidhiwa kadi katika sherehe za maazimisho zilizo fanyika jana
katika Kijiji cha Mwakizega kata ya Mwakizega Wilaya ya Uvinza.
Alisema
wanachama hao Waliamua kurudi katika Chama hicho kutokana na Shughuli
kubwa zinazo fanywa na chama hicho , ambapo mpaka sasa kuna Maendeleo
Makubwa yaliyo fanyika katika Kipindi cha Mwaka mmoja cha uongozi wa
serikali unaongozwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.
Kabourou
alisema Kwa sasa Viongozi wa chama hicho wameweka mikakati wa
kukisafisha chama hicho kwa kuondoa viongozi wote wasio na sifa
wanaokichafua sana na kuifanya CCM kuwa mpya na Serikali mpya kutokana
na Misingi iliyo wekwa na waanzirishi wa Chama hicho.
Akizungumzia
hatua hiyo, aliyekuwa mwenyekiti wa ACT wazalendo Bususnzu alisema
amegundua mapungufu makubwa katika chama cha awali hali ,iliyomshawishi
kujiunga na ccm ni pamoja na viongozi kuhamasisha misuguano kwa jamii
,ili nchi isitawalike lakini kwa awamu ya serikali ya wamu ya tano ya
John Magufuli ni kigezo cha upinzani kukubali uwajibikaji wake wenye
tija kwa wananchi.
Akizungumzia
hilo Kilembwe Omari alisema amerudi kundini akiwa na wananchama 34
kutoka chama cha ACT wazalendo ,akidai amerudi kwa baba na mama yake
akiwa na wenzake hao,sababu aminiye na kubatizwa ameokoka na anatumaini
atakuwa mumini mzuri wa chama hicho.
Akiongezea
hilo Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF,wilaya ya Kakonko Amana Ramadhani
alisema anapokea kadi kwa hiari japokuwa amekulia katika upinzani akiwa
mwenyekiti wa kina mama kwa miaka 15 wa chama cha CUF,kwa sababu ya sera
zake akijua kitawakomboa wananchi,kumbe kipo kwa ajili ya kupata ruzuku
ya serikali.
Alisema
tangu mwaka 1990 wapo wanachama wawili hali inayokwamisha jitihada za
kuleta maendeleo ,awali aliamini ujio wa UKAWA ni kuimarisha vyama
lakini kilichotokea ni ubaguzi wa udini na kugombea maslai binafsi na si
wananchi,hivyo hana budi kujiunga na ccm ili kutimiza ndoto za kuinua
uchumi .
Kwa
upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emanuel Maganga alisema kwa awamu ya
tano ya serikali ya leo,imetatua kero mbalimbali za wananchi,hususani
katika sekta ya elimu kigoma imepiga hatua 2015/16 wilaya ya kakonko
ilishika nafasi ya kwanza matokeo ya kidato cha pili na kidato cha sita
kigoma ilishika nafasi ya kwanza kitaifa.
Maendeleo
hayo ni pamoja na sekta ya miundombinu ya barabara ,miradi ya maji
zimetengwa kiasi cha sh.milioni 10 kwa kila wilaya ya kigoma kwa ajili
ya kukamilisha miundombinu ya maji iliyokuwa ikisuasua sanjari na
umalizwaji wa barabara ya Kidahwe hadi kasulu na nyakanazi Kakonko huku
Uvinza hadi Tabora fungu la fedha zimepangiwa bajeti katika mwaka wa
2016/17.
EmoticonEmoticon