Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu saba
wakiwemo viongozi na wanachama wanne wa CCM ambao ni Ndg Ally Mmbaga, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na mjumbe wa
Kamati ya Siasa ya Mkoa, Ndg Arnold Swai,
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Hai, Ndg Anastazia Innocent Malamsha, Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo
Kikuu cha Ushirika (Moshi) na Ndg Edwin
Msele, Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Kilimanjaro vilivyosababishwa
na ajali ya barabarani katika eneo la Mwika, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa
Kilimanjaro siku ya Jumapili ya tarehe 05th Februari 2017.
Ajali hiyo ilitokea
majira ya jioni ikihusisha gari ya mizigo aina ya Fuso na Toyota Hilux Surf
iliyokuwa imewabeba Viongozi wa CCM waliokuwa wakitoka katika kutekeleza
majukumu ya Chama ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika
kimkoa Wilayani Rombo na kusababisha vifo vyao.
Kutokana msiba huo, Katibu
Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Iddy Juma, familia, ndugu, jamaa, marafiki
pamoja na wanachama wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro kufuatia vifo vya Viongozi
wetu.
Wana CCM nchi nzima, tunawaombea
majeruhi kupona haraka, na tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke mahali pema roho za
Marehemu. Amina.
Imetolewa na,
HUMPHREY
POLEPOLE
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA, ITIKADI NA
UENEZI
06/02/2017.
EmoticonEmoticon