Na Emanuel Masaka, Globu ya Jamii
LIGI
ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga (Ulega Cup) imefunguliwa rasmi leo kwa
kuzikutanisha timu za Kipalang'anda kombaini Fc na Mkuranga kombaini
uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.
Mashindano
hayo yamefunguliwa na mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Firbato Sanga
ukishuhudiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega, Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Juma Abed pamoja na baadhi ya madiwani
wanaounda halmashauri hiyo.
Michuano
hiyo ambayo ilianzia ngazi ya Vijiji ilishirikisha timu 125 na baadae
kuchujwa na kubakia timu 25 ambazo zimeingia ngazi ya wilaya na mshindi
wa ligi hiyo ndio atakuwa bingwa wa wilaya.
Akizungumza
na wachezaji wa timu hizo katika ufunguzi wa michuano hiyo Mkuu wa
Wilaya hiyo Firbato Sanga alisema michezo ni udugu na ujirani mwema
hivyo aliwatakia michezo mwema.
Akizungumzia
michuano hiyo Mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega amesema kuwa ni
matarajio yake michuano hiyo itakwenda vyema na lengo lake kubwa
nikuona wanapata vijana wenye vipaji na watakaoweza kuipaisha Mkuranga.
"Nimatarajio
yangu mambo yatakwenda kama nilivyopanga na kama mnavyoona wenyewe
waandishi wa habari vijana wa kutoka Mkuranga ndio wanaocheza "alisema
Ulega
Amesema
tangu awali alisha kataa timu hizo kukodi watu Kutoka nje ya Mkuranga
na anashukuru Mungu hayo yamezingatiwa na katika michuano hiyo mshindi
ndio atakuwa bingwa wa Wilaya.
Amesema
kuwa ana matumaini makubwa kwamba kupitia ligi hiyo watapatikanika
vijana wenye uwezo ambao wataweza kuchukuliwa na timu kubwa.
Aidha
amesema kuwa michezo ni Afya ,ajira,na upendo kwani kupitia mashindano
hayo watakuwa wametengeneza ujirani mwema hivyo watumie fursa hiyo
kudumisha Umoja na mshikamono miongoni mwao.
Mchezo
huo ulimalizika kwa goli moja lililofungwa na mchezaji wa timu ya
Mkuranga Kombaini,Abdallah Mohamed katika dakika ya kumi kipindi cha
kwanza.
Mbunge
wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) katika ufunguzi wa Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga
(Ulega Cup) uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga
mkoani Pwani
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga,Firbato Sanga akizungumza na wachezaji wa timu
za Kipalang'anda kombaini Fc na Mkuranga kombaini katika ufunguzi wa
Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga (Ulega Cup) uliofanyika katika
uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga,Firbato akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mkuranga,Juma Abed katika uwanja wa shule ya msingi
Mkuranga mkoani Pwani
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga,Firbato Sanga akiwa kwenye picha ya pamoja na
wachezaji wa timu ya Mkuranga Kombaini pamoja viongozi mblimbali katika
uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga,Firbato Sanga akiwa katika picha ya pamoja na
wachezaji wa timu ya Kipalang'anda kombaini Fc katika uwanja wa shule
ya msingi Mkuranga mkoani Pwani.
.Sehemu
ya mashabi wa timu ya Kipalang,anda kombaini Fc na Mkuranga kombaini
wakiwa wakishuhudia mtanange katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga
mkoani Pwani
.Mchezo
ukiendelea ambapo mchezo huo ulimalizika kwa goli moja lililofungwa na
mchezaji wa timu ya Mkuranga Kombaini,Abdallah Mohamed katika dakika
ya kumi kipindi cha kwanza.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
Pwani.
EmoticonEmoticon