**sasa uzalishaji mwaka mzima
**Mtaka asema ni aibu Simiyu kuomba chakula wakiwa na maji tele Busega
BENKI
ya NMB imekubali kutoa fedha kwa ajili ya kujenga 'skimu' kubwa ya
mfano ya umwagiliaji katika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
"Maji
ni raslimali muhimu sana inayotoa uhakika wa kuvuna pamoja mbali ya
pembejeo na uhifadhi', alisema Seif Ahmed, afisa mkuu upande wa biashara
ya kilimo (Agribusiness) mwishoni mwa wiki.
"Mkuu
wa Mkoa ninakupongeza wewe na timu yako kwa nia ya kuwaletea wananchi
wa Simiyu maendeleo, " alisema na kuongeza, "Ninawahakikishia kuwa
tutawapatia mkopo huo."
Ahmed aliahidi kufanya kazi pamoja na Mkoa wa Simiyu kuhakikisha mradi unaleta mabadiliko ndani ya jamii.
Afisa
Mwakilishi wa Serikali katika NMB, Domina Feruz, alisema kilimo cha
umwagiliaji kitatoa uhakika wa mavuno na kuwapo uhakika wa marejesho ya
mkopo na chakula muda wote wa mwaka", alisema Afisa huyo.
*NMB KUUNGANISHA NGUVU*
Alisema
kuwa NMB iko tayari kuwaunganisha na mfadhili wa kimataifa ambaye
atawapatia ufadhili mkubwa zaidi wa kifedha alimradi wanunue zana za
kilimo kutoka kwenye kampuni hiyo.
Ahmed
alisema MMB iko tayari kushirikiana na washirika wengine kama PASS,
katika uandaaji wa mpango wa mradi pamoja na Serikali ya Mkoa wa Simiyu
ili mradi uanze mara moja.
"Ukweli
ni kwamba tukiendelea kusubiri mvua ili tuvune, ni vigumu kupiga hatua
kubwa ya maendeleo na mabenki yanatoa fedha zao kwa woga wa kuzipoteza
endapo mvua haitanyesha," alisema.
Ahmed
aliongeza kuwa skimu ya umwagiliaji itawaunganisha wakulima sio tu
kuwapa sauti moja bali pia kusafirisha mazao yao katika masoko ya nje ya
nchi (export markets).
Tanzania,
katika utawapa wa Mwalimu Nyerere, iliwahi kuwa na kampuni ya uuzaji wa
mazao ya kilimo katika masoko ya kimataifa, GAPEX, ambayo ililiwezesha
Taifa kupata fedha nyingi za kigeni.
*KUSHIRIKI UCHIMBAJI MITARO*
"Mimi
pamoja na Kamati yangu ya Ulinzi na Usalama mtupangie Kata za kwenda
kushiriki uchimbaji wa mitaro ya umwagiliaji, " alisema RC Mtaka.
RC Mtaka alisema Mh Rais Magufuli atawashangaa endapo wataomba chakula wakati wana maji tee pale Busega.
Mh
Rais atatushangaa. Tumeikataa hii aibu Simiyu kuomba chakula wakati
tuna maji tele Busega, nitashirikiana na wananchi mimi na Kamati yangu
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiwa sehemu ya mchango wetu," alisema.
*ENEO LA MRADI*
Mradi wa kujenga miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji maji utafanyika
katika Kata sita za Wilaya ya Busega zenye ukubwa wa hekta 1,500.
Hata
hivyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Busega, ambaye pia ni Diwani wa
Kata ya Kiloleli, Vumi Magoti, ameshauri kuangalia uwezekano wa kupanua
mradi kufikia hekta 6,000.
"Inawezekana kupata impact kubwa zaidi endapo tutaweza kuongeza eneo la mradi,"alisema.
Alisema
wananchi wa Busega huwa wanachanga fedha kumlipa mtu awaletee mvua bila
kuwa na uhakika, "huu mradi una uhakika wa kuleta maji, watahamasika
kushiriki kuchimba mitaro," alisema Bw Magoti.
*SKIMU KUONGEZA UZALISHAJI WA MPUNGA*
Katika hotuba yake ya ufunguaji wa mkutano huo wa kazi, RC Mtaka
alisema, pamoja na mazao mengine, mradi unalenga kuzalisha zao la
mpunga.
*AWATAKA NMB KUFUNGUA TAWI BUSEGA*
Aliwataka
NMB kuharakisha kufungua tawi lao Wilayani Busega kabla mradi haujaanza
ili kukabiliana na ongezeko la uhitaji wa huduma za kibenki wilayani
humo hasa baada ya mradi kuanza.
Katika
ziara yake, Mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu alikubaliwa kupata mkopo mkubwa
kutoka Benki ya Maendeleo ya TIB. Mkopo huo utasaidia miradi mbalimbali
ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji katika kiwanda cha
chaki.
Miradi
mwingine ni ujenzi wa Kiwanda cha uzalishaji wa vifaa vya hospitali
vinavyotokana na mazao ya pamba ambapo TIB itawapatia Sh150m kwa ajili
ya maandalizi ya Awali ya mradi.
Vilevilena
upimaji wa Benki hiyo itawakopesha fedha kwa ajili ya mradi wa upimaji
wa viwanja vya makazi, biashara na taasisi katika eneo la Mperani
katika Halmashauri ya Bariadi.
*KUUNGANISHA NGUVU ZA KITAASISI*
"Tumeamua kujenga mkoa mpya wa kiuchumi Simiyu, tunawaomba TIRDO, TFDA,
TBS, TEMDO, CARMATEC, TIB, SIDO pamoja na Simiyu, tuungane kujenga
viwanda kuifanya Tanzania ya viwanda iwe halisi.
Mh
Mtaka na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, walimaliza
ziara yao mwishoni mwa wiki, ziara iliyokuwa na mafanikio makubwa
katika jitihada zao za ujenzi wa viwanda na kuanzisha kilimo cha
umwagiliaji.
Walitembelea TBA, TBA, NMB, TIRDO, SUMA-JKT na Baraza la uwezeshaji kiuchumi la Taifa, NEEC.
EmoticonEmoticon