Na Woinde
Shizza,Arusha
Halmashauri ya jiji la Arusha imeokoa zaidi ya shilingi milioni
mia tatu sitini na nne zilizokuwa zitumike kwa ajili ya kuwapa
wakandarasi kwa jili ya kujenga madarasa baada yake kamati za shule
kupewa jukumu la kusimamia ujenzi wa madarasa hayo badala ya
mkandarasi
Hayo yamebainishwa na meya wa halmashaur i ya jiji la Arusha Kalist
Lazarowakati akiongea na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa
halmashauri yake wamekaa chini na kuona kuliko fedha hizo zipewe wakandasi ili
wajengee madarasa ni bora fedha za ujenzi wa madarasa zipelekwe katika
kamati za
shule pamoja na bodi za shule ili wasimamie ujenzi
huo
Alisema kuwa sasa ivi halmashauri imetoa shilingi bilioni moja
laki nne kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 56 ya shule za msingi na fedha
zote zilishapelekwa katika kamati za shule ili waweze kusimamia
ujenzi mpaka ukamilike.
“zamani tulikuwa tunatumia wakandarasi kwa kutangaza tenda kwa ajili
ya kujenga madarasa ya shule za msingi ,lakini tangu tuanze
kujenga madarasa kwa kupitia kamati za shule na sio wakandarasi tumekuwa tunaokoa
milioni mia tatu sitini nne ambazo tumeziokoa tungetumia wakandarasi
zote zingeingia katika mfuko wa mkandasi sasa ndio maana tumeamua
kumtumia kamati za shule kwa shule za msingii “alisema Kalist
Aidha alisema kuwa jiji la Arusha kumekuwa na ongezeko kubwa la
watoto ambao wanaandikishwa darasa la kwanza tuofauti na mwaka huliopita
kwani tangu zoenzi limeanza adi kufikia sasa wameshaandikisha wanafunzi wa
darasa la kwaza zaidi ya elfu 12000 tofauti na mwaka uliopita 2016 ambapo
watoto elfu
tisa mia sita na mia waliandikishwa kuingia darasa la kwanza ,
ambapo alisema bado wanaendelea kuandikisha watoto adi mwezi march ili watoto
wote waweze kwenda shule
Alisema kuwa kutokana na kuwepo na watoto wengi waliojiandikisha
kumekuwa na upungufu wa madarasa hivyo halmashauri imejenga madarasa 56
kwa ajili ya watoto hao wapya na kukarabati madarasa manne ya shule ya
msingi ambayo yatasaidia kabisa kumaliza tatizo hili,ambapo alisema kuwa pia
madarasa hayo yanaitaji madawati na hadi sasa halmashauri imeshatoa fedha kwa
ajili
ya madawati 1380 ambayo watoto hao watakalia katika madarasa hayo
mapya hivyo wanaimani kuwa watoto wote wanaoanza darasa la kwanza
wataingia madarasani na kukaa katika madawati na kusoma vizuri kama
vile
inavyotakiwa.
Akifafanua kuhusu wanafunzi wa shule za sekondari alisema kuwa jiji
la Arusha lilifaulisha kwa asilimia 92% wanafunzi wanaoingia kidato cha
kwanza na kukakuwepo na upun gufu wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi hao
lakini jiji limeshajipanga vyema na imeanza kujenga madarasa 25 kwa ajili ya
shule
za sekondari na kiasi cha shilingi milioni 700 zimeshatumwa katika
bodi za shule hizo na wanaimani adi ifike mwisho wa mwezi huu wanafunzi
wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza wataingia madarasani na
kuendelea na
masomo kama kawaida.
“napenda ku sema kuwa hakuna mtoto ambaye amefaulu kuingia kidato
cha kwanza ataacha kuingia darasani ifikapo mwisho wa mwezi huu
madarasa yatakuwa tayari na wanafunzi wote waliofaulu wataenda shule “alisema
kalist
EmoticonEmoticon