LIGI
kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena kesho Ijumaa kwa mchezo
Na. 129 utakaozikutanisha timu za African Lyon na Young Africans kwenye
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam utakaochezeshwa na
Mwamuzi, Ludovic Charles kutoka mkoani Tabora akisaidiwa na John
Kanyenye wa Mbeya (Mshika Kibendera Na. 1) na Alnord Bugado wa Singida
(Mshika Kibendera Na. 2), Mwamuzi wa Akiba – Mezani anatarajiwa kuwa
Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam.
Jumamosi
Desemba 24, 2016 kutakuwa na mechi sita ya Mbeya City na Toto African
kwenye Uwanja wa Sokoine jijiji Mbeya katika mchezo Na. 130
utakaosimamiwa na Kamishna George Komba wa Dodoma wakati Mwamzi wa kati
atakuwa Shakaile ole Shangalai wa Pwani huku wasaidizi wake wakiwa ni
Khalfan Sika pia wa Pwani na Vecent Milabu wa Morogoro. Mwamuzi wa akiba
atakuwa Cherles Mwamlima.
Mchezo
Na. 131 utazikutanisha timu za Kagera Sugar na Stand United katika
Uwanja wa Kaitaba, uliko Kagera ambako utasimamiwa na Kamishna Nassoroi
Hamduni wa Kigoma huku Mwamuzi akiwa ni Jacob Adongo wa Mara akisaidiwa
na Joseph Masija na Robert Luhemeja kutoka Mwanza na Mezani atakuwa
Jonesia Rukyaa wa Kagera.
Ndanda
itaendelea kubaki nyumbani kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara
na baada ya kucheza na Simba juma lililopita na kupoteza mchezo huo,
safari hii inaikaribisha Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo Na. 132
utakaosimamiwa na Kamishna Jimmy Lengwe wa Morogoro wakati Mwamuzi
atakuwa Andrew Shamba wa Pwani akisaidiwa na Haji Mwalukuta wa Tanga na
Jeremiah Simon wa Dar es Salaam. Mezani atakuwa Abubakar Mtulo.
Mchezo Na. 133 utafanyika Uwanja wa Uhuru, kati ya
Simba na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
utasimamiwa na Tito Haule wa Morogoro na kuchezeshwa
na Mwamuzi Hans Mabena wa Tanga akisaidiwa na Omari Kambangwa wa Dar es
Salaam na Khalfan Sika wa Pwani wakati Mbaraka Rashid wa Dar es Salaam
atakuwa Mwamuzi wa Akiba – mezani.
Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Azam FC ya Dar es Salaam k
Mwadui atakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye
Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga kwenye mchezo huo Na. 135,
utakaosimamiwa na Kamishna Staricko Nyikwa wa Singida na mw
aamuzi atakuwa ni Emmanuel Mwandembwa akisaidiwa na
Abdallah Uhako na Agnes Pantaleo wote wa Arusha na mezani anatarajiwa
kuwa Ezekiel Mboi wa Shinyanga.
Desemba 26, Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons
ya Mbeya kwenye Uwanja wa Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani katika
mchezo Na 136 na
Manyama Bwire wa Dar es Salaam atakuwa Kamishna
wa mchezo huo wakati Mwamuzi ni Forentina Zabron wa Dodoma akisaidiwa na
Hassan Zani wa Arusha na Silvester Mwanga wa Kilimanjaro. Mwamuzi wa
akiba - Mezani atakuwa Andrew Shamba wa Pwani.
Desemba
28, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili ambako Young Africans ya Dar es
Salaam itakuwa mwenyeji wa Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Uhuru
jijini katika mchezo Na. 137 ambako Juma Chiponda wa Tanga atakuwa
kamishna wa mchezo huo.
Mwamuzi wa kati katika mchezo huo atakuwa Eric
Onoca wa Arusha akisaidiwa na Michael Mkongwa wa Njombe na Janeth Balama
wa Iringa. Mwamuzi wa akiba atakayekaa mezani atakuwa Mwanahamisi
Matiku wa Dar es Salaam.
Kadhalika
siku hiyo, Majimaji ya Songea itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro
kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Mvomero katika mchezo Na. 138
utakaosimamiwa na Kamishna Pius Mashera wa Dodoma, utachezeshwa na
Mathew Akrama kutoka Mwanza akisaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na
Gasper Ketto wa Arusha. Mwamuzi wa akiba atakuwa Selemani Kinugani.
Kadhalika
Desemba 29, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili. Ruvu Shooting ya Pwani
inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa
Uhuru Dar es Salaam katika mchezo ambao mwamuzi atakuwa Alex Mahagi wa
Mwanza.
Katika
mchezo huo Na. 139, Mahagi atasaidiwa na Ferdinand Chacha pia wa Mwanza
na Rashid Zongo wa Iringa huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Hellen Mduma
wa Dar es Salaam. Kamishna wa mchezo atakuwa Peter Temu wa Arusha.
Azam
itavaana na Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo Na. 140
utakaosimamiwa na Elizabeth Kalinga wa Mbeya huku Mwamuzi akiwa ni Jimmy
Fanuel wa Shinyanga huku wasaidizi wake wakiwa ni Makame Mdog pia wa
Shinyanga na Abdallah Mkomwa wa Pwani huku Kassim Mpinga akiwa ni
mwamuzi wa akiba.
Kamishna
anatarajiwa kuwa Nassib Mabrouk wa Mwanza na Mwamuzi ni Isihaka Mwalile
na wasaidizi wake ni Hellen Mduma na Omary Kambangwa – wote kutoka Dar
es Salaam. Julius Kasitu wa Shinyanga anatarajiwa kuwa Mwamuzi wa Akiba.
Kadhalika
siku ya funga mwaka, Mbeya City inatarajiwa kucheza na Mbao FC kwenye
Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika Mchezo Na. 143 ambao msimamizi wa
mchezo atakuwa Joseph Mapunda wa Ruvuma.
Mwamuzi
katika mechi hiyo anatarajiwa kuwa Hussein Athuman wa Katavi wakati
wasaidizi wake watakuwa ni Lulu Mushi wa Dar es Salaam na Nicholaus
Makaranga wa Morogoro. Mwamuzi wa Akiba Mezani atakuwa Mashaka
Mwandembwa wa Mbeya.
Januari
mosi kutakuwa na michezo miwili tu ya kukaribisha Mwaka Mpya ambako
Toto African ya Mwanza itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo Na. 144 utakaosimamiwa na Jovin
Bagenda wa Kagera. Mwamuzi atakuwa Israel Nkongo sambamba na wasaidizi
wake Soud Lila na Frank Komba, wote wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa akiba
mezani atakuwa Mathew Akrama wa Mwanza.
Pia
African Lyon ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu katika mchezo
Na. 142 utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Kamishna atakuwa
Hamisi Kitila wa Singida wakati Mwamuzi anatarajiwa kuwa Selemani
Kinugani wa Morogoro wakati wasaidizi wake ni Omary Juma wa Dodoma na
Agnes Pantaleo wa Arusha wakati mezani atakuwa Shafii Mohammed wa Dar es
Salaam
Mara
baada ya michezo hiyo, Ligi Kuu ya Vodacom itasimama kwa wiki mbili
kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Januari
mosi, mwaka huu.
EmoticonEmoticon