Mmoja wa abiraia aliyekosa usafiri katika kituo cha mabasi Ubungo akiwa amekaa chini na mtoto wak mara baada ya kuchoka na kadhia ya kukosa usafiri.
Sehemu ya kituo cha mabasi Ubungo ikionekana kwa juu majira ya saa mbili asubuhi huku abiria wakiwa wengi kuliko magari
Wananchi wakiwa wamemzunguka afisa wa SUMATRA akiwa amezungukwa na wasafiri mbalimbali ambao wamekosa usafiri
Abiria waliokosa usafiri wakiwa kando ya kituo cha Polisi. Usalama barabarani wakisubiri kupewa huduma
Sehemu ya kituo cha mabasi Ubungo ikionekana kwa juu majira ya saa mbili asubuhi huku abiria wakiwa wengi kuliko magari
Abiria wakiingia katika daladala,inayofanya safari zake Gongolamboto na Simu 2000 likiwa katika kituo kikuu cha mabasi ubungo likipakianabria wa kwenda mkoa wa Kilimanjaro.
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii
Hali ya usafiri imeendelea kuwa tete katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo kutokana kuwepo kwa uhaba wa usafiri kwa wasafiri wanaokwenda mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania na Nyanda za juu kusini.
Globu ya jamii ilifika katika kituo hicho cha mabasi na kujionea ni jinsi gani wasafiri wakipata taabu ya kupata mabasi,licha ya mammlaka ya usafirishaji majini na nchi kavu (SUMATRA) kuomba wenye magari yenye vigezo kufika katika kituo hicho kwa ajili ya kupewa kibali cha kusafirisha abiria mikoani.
Akizungumza na globu ya Jamii,Mwananchi mmoja wa wasafiri anayekwenda Rombo mkoani Moshi, Elikunda Towo, amesema kuwa walikuwa wakihitaji usafiri tangu jana lakini wamekosa .
"Magari yaliyopo hapa yanagoma kupakia abiria yakisema kuwa ni mabovu na hawana uhakika wa safari ,hivyo hawawezi kupakia lakini ghafla unaona basi limejaa na linaondoka, sasa tunajiuliza hizo basi abiria wanapakilia kwa staili ipi,huku Sumatra wakiwa wamejazana hapa katika kituo cha mabasi" anasema huku akihoji abiria huyo .
Ameongeza kuwa ni vyema serikali ikandeleza umakini katika kusimamia magari hayo,ili abiria waweze kusafiri kwa uhakika kuliko ilivyo hivi sasa.ambapo kundi kubwa la abiria likiwa linakaa hapo Kituoni Ubungo bila mafanikio yoyote ya kupata usafiri.
Abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jamila Mwampulule amesema kuwa walifanikiwa kukata tiketi katika basi la Rungwe, lakini ilivyofika asubuhi wakajikuta wanarudishiwa nauli kwa kuambiwa basi loa ni bovu huku kukiwa hakuna usafiri mwingine mbadala wa kwenda Mbeya.
EmoticonEmoticon