Wachezaji wa timu za Bandari ya Dar es Salaam na Makao Makuu wakichuana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari Tanga ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47
Wachezaji wa timu za Bandari ya Dar es Salaam na Makao
Makuu wakichuana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye
uwanja wa Bandari Tanga ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47
Wachezaji wa kuvuta kamba timu ya Bandari ya Tanga wakichuana dhidi ya Makao Makuu mchezo umalizika kwa Tanga kuibuka na ushindi wa seti 2-0 mchezo uliochezwa viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlaly mjini Tanga
TIMU
ya Mpira wa Pete ya Bandari ya Tanga leo wameweza kuibuka na ushindi wa mabao
43-16 dhidi ya Bandari ya Mtwara kwenye michuano ya Bandari inayoendelea mjini
Tanga.
Mchezo
huo ambao ulichezwa kwenye viwanja vya Bandari mjini hapa ambapo mpaka timu
zote zinakwenda mapumziko Bandari Tanga ilikuwa ikiongozwa kwa mabao 23 -17
dhidi ya Mtwara.
Halikadhalika
Tanga wakiweza kuibuka pia na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Makao Makuu kwenye mchezo wa mpira wa miguu
uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini hapa.
Katika
mchezo mwengine uliochezwa kwenye uwanja huo timu ya Bandari ya Dar es Salaam
iliweza kuibuka na ushindi dhidi ya Makao Makuu kwa mabao 36-13.
Wakati
huo huo,Timu ya Bandari ya Dar es Salaam imeweza kuibuka na ushindi wa vikapu
50 -47 dhidi ya Makao Makuu kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye
dimba hilo la Bandari mjini hapa.
Kwenye
mchezo mpira wa miguu uliozikutanisha Bandari Mtwara na Maziwa Makuu ambapo
timu hizo mpaka dakika 90 zilijikuta zikigawana pointi moja moja baada ya kutoka
sare ya kufungana bao 1-1.
Ili
kuonyesha wana umahiri mkubwa kwenye michezo Bandari Tanga wanaume waliweza
kuibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Makao Makuu kwenye mchezo wa kuvuta
kamba.
Wakati
wanaume wakiibuka na ushindi huo wanawake nao waliweza kuwaunga mkono wenzao
kwa kuibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Makao makuu kwenye mchezo wa kuvuta
kamba uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popatlaly.
Mashindano
hayo ambayo yalifunguliwa jana na Mkurugenzi wa Bandari nchini (TPA) Deusdedit
Kakoko ambaye aliwataka wanamichezo hao kuzingatia nidhamu na maarifa kwenye
michezo yao ili kupata ushindi.
EmoticonEmoticon