Na Ally Daud -MAELEZO
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (2017-22) wa
Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Hayo yamesemwa jana na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(Maendeleo ya Jamii) Bi. Siaba Nkinga katika mkutano na waandishi wa
habari, ambapo alisema uzinduzi huo unatarajia kufanyika Desemba 13
mwaka huu Jijini Dar es Salaam
“Mpango huu jumuishi wa miaka
mitano utakaouzinduliwa umezingatia nguzo kuu mbili, ambazo ni kuzuia na
utoaji wa huduma kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia”
alisema Bi. Nkinga
Alisema kuwa mpango kazi huo
unatarajiwa kutoa msukumo mpya katika kuwezesha utekelezaji majukumu
ikiwemo kutetea, kushauri na kutoa elimu kwa umma ili kuongeza uelewa
kwa jamii kuhusu athari za ukatili kwa wanawake.
Kwa mujibu wa Nkinga alisema kuwa
utafiti uliofanywa na Shirika la Kuhudumia Watoto Ulimwenguni (UNICEF)
wa mwaka 2015, unaonyesha kuwa Tanzania ina asilimia 3.5 ya watoto wa
umri wa miaka 7 – 17 walio nje ya shule kutokana na sababu mbalimbali
za ukatili.
Alibainisha Vitendo vya ukatili
wa kijinsia vilivyoshamiri zaidi ni pamoja na vipigo, ubakaji, ulawiti,
mauaji ya vikongwe, na watu wenye ualibino, usafirishaji haramu wa
binadamu, kutelekeza familia, udhalilishaji, ukeketaji, mimba na ndoa za
utotoni.
EmoticonEmoticon