Mkuu Wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Alexander
Mnyeti(kushoto0 wakiwalia katika kijiji cha Nkoasenga kwa ajili ya
kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa maji Makilenga.
Mhandi
wa Maji Happy Mrisho (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya mradi kwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha(hayupo pichani) wakati wa kikao cha kutafuta
ufumbuzi wa mgogoro wa Maji Makilenga.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Makilenga waliohudhuiria kwenye Mkutano wa hadhara.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alaxander Mnyeti akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga kwenye Mkutano wa hadara.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (aliyesimama mbele) akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga kwenye Mkutano wa hadhara
Baadhi
ya Wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga wakifurahia makubaliano
yaliyofikiwa katika ya Serikali na kijiji hicho ya kulipa Tsh 1500 kwa
huduma ya maji mwezi mzima kwa wanaotumia mabomba ya Kijiji .
……………………………………………………………….
Nteghenjwa Hosseah – Arumeru
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe .
Mrisho Mashaka Gambo amemaliza mgogoro wa muda mrefu uliodumu zaidi ya
miaka mitatu kati ya Bodi ya Maji ya Makilenga na wananchi wa Kijiji cha
Nkoasenga, Kata ya Leburuki Wilayani Arumeru.
Utatuzi wa mgogoro huo ulifikiwa
kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Nkoasenga baada
ya Mhe. Gambo kuwashirkisha wananchi wa aneo hilo katika kutatua
changamoto hii iliyoathiri wananchi zaidi ya hamsini elfu wa kijiji hiki
pamoja na vijiji vingine ishirini na sita vinavyotegemea mradi huo.
Wananchi hawa waliofungiwa maji
kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa baada ya kufanya uharibifu wa miundombinu
ya Maji pamoja na kuweka kinyesi kwenye mabomba walionyesha kuchoshwa na
adha hiyo ya kufuata maji umbali mrefu na kwa gharama kubwa zaidi
ilihali maji yanapatikana katika Kijiji chao na walionyesha hali ya
kutaka muafaka wa jambo hili ili kuendelea kupata huduma ya maji kama
ilivyokuwa hapo awali.
Akiongea katika Mkutano huo baada
ya mazungumzo na viongozi wa Kijiji pamoja wananchi Mkuu wa Mkoa Mhe.
Mrisho Gambo alisema katika kutoa huduma ya Maji Vijijini tunaongozwa na
Sera ya Maji ya mwaka 2002 inayotaka kuchangia hudma za maji na sio
kununu Maji hivyo kila kaya inawajibu wa kuchangia kiasi kidogo cha
Fedha ili kuwezesha huduma hii iendelee kutolewa siku zote.
“Tunafahamu kwamba maji haya
yanaanzia kwenye Kijiji hiki na wakazi wa Nkoasenga ndio walinzi wakuu
wa mradi huu na wanastahili kupewa upendeleo wapekee katika kutumia
maji haya ili wendelee kutunza mradi huu wa Maji, ni wazi kuwa vijiji
vya ukanda wa chini haviwezi kupata Maji endapo tu wana Nkoasenga
wataharibu mradi huu wa maji mtiririko”, Alisema Mhe. Gambo.
Aliongeza kuwa umuhimu huu wa
nyie kuwa Kijiji mama cha mradi huu hauwapi Kinga ya kutokuchangia
gharama za maji, hivyo nataka mniambia mnaweza kuchangia kiasi gani
kadiri ya uwezo wenu na baada ya makubalino haya mtalipia gharama za
maji kwa mwezi na sio kwa mwaka tena kama mlivyokuwa mnafanya hapo
awali”.
Awali akizungumza katika Mkutano
huo Mhandisi wa Maji Bi. Happy Mrisho alisema “mradi wa maji Makilenga
uliibuliwa na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga na baada ya thatmini ya
awali ilonekana kuwa mradi ni wa gharama kubwa hivyo usingekidhi vigezo
vya kiufadhili kama ungekua mradi wa kijiji kimoja na ili kukidhi vigezo
vya kupata fedha toka kwa wafadhili ililazimu kuongeza wanufaika kutoka
vijiji 26 na utekelezaji ukaendelea”.
Aliongeza kuwa baada ya mradi
kukamilika iliundwa Kamati tendaji ya Makilema ambayo ndiyo inayosimamia
mrdai huu na Madiwani na wenyeviti wote wa vijiji waliingia makubaliano
ya kuchangia Tsh 10 kwa ndoo lakini baada ya muda mfupi wanakijiji wa
Nkoasenga walikiuka makubalino hayo na kudai watalipa Tsh 5000 kwa
mwaka na hawewezi kulipa kwa ndoo kwa kuwa maji hayo ni mali ya Kijiji.
Anderson Sikawa ni Diwani wa Kata
ya Leburuki kilipo kijiji cha Nkoasenga alisema hawakatai kuchangia
huduma za Maji lakini kutokana na hali duni ya wananchi wa eneo hilo
hawawezi kulipa kwa ndoo hivyo wanahitaji kufanya mapitio ya gharama za
Maji ili kuendana na hali ya wana Nkoasenga ambayo pia itawaongezea ari
wakazi hao kulinda mradi huo kwa manufaa ya vijiji vingine pia alitoa
tuhuma kwa Bodi ya Makilenga kwa matumizi mabaya ya Fedha za maji.
Katika kutoa mapendekezo ya kiasi
stahiki cha kuchangia huduma ya Maji Ndg. Afred Masao ambaye ni
mwananchi wa Kijiji cha Nkoasenga aliwakilisha wananchi wote wa Kijiji
hicho alisema kuwa wananchi wako tayari kuchangia kwa mwezi lakini
uwezo wao ni Tsh 1500 na sio Ths 3000 kama ilivyopendekezwa kwenye
vikao vya ndani katika ya Mkuu wa Mkoa na viongozi wa Kijiji.
Rc Gambo alihitimisha Mkutano huo
kwa kukubaliana na mapendekezo ya wananchi kuwa watalipia Tsh 1500 kwa
mwezi kwa wale wanaotumia mabomba ya Kijiji na kwa wale wenye mabomba
nyumbani watalipia kadiri ya matumizi yao kwa mwezi na wote
watafungiwa Mita za Maji pia aliwaagiza wananchi hao kulipia gharama
hizo Halmashauri na sio kwa Kamati ya Maji Makilenga kama awali.
Mradi wa Maji wa Makilenga
ulianza mwaka 2011 kwa lengo la kutoa huduma ya Maji na kuhudmia Kata
nne na vijiji 27; Ulifadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa kutoa kiasi cha
Tsh Bil 3.7, OIKOS pamoja na nguvu za wananchi. Mradi huu unaendeshwa na
Jumuiya ya watumiaji maji ya Makilenga ambayo ina jukumu na mamlaka ya
Kisheria kusimamia mradi huu wa maji.
EmoticonEmoticon