-Usalama wa Wanawake
kufuatia Mabadiliko ya Tabia Nchi
Ukatili dhidi ya wanawake ni uvunjaji mkubwa wa haki
za msingi za binadamu na tishio kwa mamilioni ya wasichana na wanawake duniani
kote. Takribani mwanamke mmoja kati ya wanawake watatu duniani amekuwa
akipigwa, kulazimishwa kufanya ngono, au kunyanyaswa vinginevyo katika maisha
yake. Jamii nzima imeathiriwa na ukatili ambao unaweza kuwa wa kimwili, kingono
(unyanyasaji, kulazimishwa au kubaguliwa) na kisaikolojia (kunyanyaswa kwa
maneno au kwa hisia, kama vile kuonewa au kutengwa).
Katika siku hii ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili
Dhidi ya Wanawake, UNESCO inaangazia mabadiliko ya tabia nchi na uhaba wa
rasilimali kama sababu za kuchochea ukatili dhidi ya wanawake – nyumbani,
mitaani, wakati wa majanga asilia yanayosababishwa na tabia nchi.
Mabadiliko ya tabia nchi yanazidisha tishio - yanaweza
kuongeza uhamaji na kukosa makazi kwa watu na kuchangia katika kutokuzalishwa
kwa mazao au mafuriko, kuongeza msukumo nyumbani na katika utafutaji wa
riziki. Utafiti unaonyesha kwamba
wanawake wanawajibika kwa asilimia 65 ya uzalishaji wa chakula katika kaya huko
Asia, kwa asilimia 75 katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na kwa asilimia
45 huko Amerika ya Kusini. Mara nyingi, ni wajibu wa kiutamaduni wa wanawake
unaowaweka katika hatari kubwa dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabia nchi – na
kwa hiyo kujikuta wakiwa katika mazingira yenye uwezekano wa kufanyiwa ukatili
wanavyotembea maili nyingi kila siku kutafuta chakula, maji na kuni au baada ya
kukosa makazi au kupata umasikini kutokana na majanga. Kukosa njia za
kujitafutia riziki na umasikini kunaweza pia kusababisha ukatili nyumbani
kutokana na msukumo wa kiuchumi, pamoja na kuendelea kwa muda mrefu kwa
mienendo ya ukeketaji wa wanawake na ndoa za utotoni.
UNESCO inashiriki kikamilifu katika kuimarisha ujasiri
wa kukabili mabadiliko ya tabia nchi, ujumuishaji wa mkabala wa kijinsia katika
utendaji wake wote. Kwa kutumia ushirikiano na mipango ya kibunifu, UNESCO
inaendeleza fikra inayodai kuwa wanawake na wasichana ni muhimu katika
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, hasa, kwa mfano, mipango ya kusimamia
maji na utayari wa kukabiliana na majanga.
Tunafahamu kwamba uzalishaji wa gesi ukaa unaiathiri
sayari ya dunia. Tunapaswa pia tutambue kwamba mabadiliko ya tabia nchi
yanaathiri maisha ya wasichana na wanawake duniani kote. Tunapokuwa tupo tayari
kuanza kutekeleza Mkataba wa Tabia Nchi wa Paris na kujiandaa kwa ajili ya
mafanikio ya COP22 huko Marrekech, tusiisahau nusu ya idadi ya watu wetu na uwezo
wao mkubwa wanaouwakilisha. Wanawake lazima wawe katika kiini cha utatuzi wote
wa mabadiliko ya tabia nchi.
EmoticonEmoticon