BARAZA LA WAHITIMU WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE LAKUTANA KUJADILI MUSTAKABARI WA CHUO

November 25, 2016

 Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila (kushoto), akihutubia wakati akifungua Baraza la Wahitimu wa chuo hicho, Dar es Salaam leo.
 Katibu wa Baraza la Wahitimu wa chuo hicho, Jumanne Muruga (kushoto), akihutubia katika baraza hilo.
 Mwenyekiti wa Baraza hilo, Simon Simalenga (katikati), akiongoza baraza hilo. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila na kushoto ni Katibu wa baraza hilo, Jumanne Muruga.

 Diwani wa Kata ya Mbezi, Humphrey Sambo ambaye aliwahi kuwa Rais wa Serikali ya chuo hicho (MASO), akichokoza mada katika baraza hilo.
 Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
 Meza kuu ikimba wimbo wa taifa.
 Wanachuo wakiimba wimbo wa taifa.
 Taswira ya mkutano huo.
 Baraza likiendelea.
Majadiliano yakiendelea.
 Wanafunzi wakisikiliza mada kwa makini.
 Taswira ya ukumbi.
Mwanahabari Suleiman Msuya ambaye ni muhitimu wa chuo hicho, akichangia mada katika baraza hilo.
Wanafunzi wakisikiliza mijadala.
Vyeti vikitolewa
Picha ya pamoja.



Na Dotto Mwaibale


MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amesema chuo hicho kipo katika mpango wa kujenga miundombinu mizuri ili wanafunzi wapate elimu katika mazingira bora.


Profesa Mwakalila ameyasema hayo wakati akifunga Baraza la Wahitimu wa chuo hicho lililofanyika chuoni hapo Dar es Salaam leo kutokana na maombi ya wahitimu wa chuo hicho wanaounda baraza hilo kulalamikia miundombinu katika shule hiyo.


"Ni kweli tunachangamoto kubwa ya miundombinu hapa chuoni lakini tupo katika mpango wa kuijenga kwani tayari Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wameanza kuandaa michoro ya majengo na fedha tunategemea kupata kutoka kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya ujenzi na sasa tupo katika mazungumzo nao" alisema Mwakalila.


Alisema miundombinu  hasa madarasa na hosteli ni changamoto kubwa kwani kutokana na sifa ya chuo hicho wanafunzi wamekuwa wakiongezeka kila mwaka hivyo kusababisha changamoto hiyo ambayoitakwisha muda si mrefu.


Akizungumzia kuhusu la Baraza la Wahitimu alisema lilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya chuo na lipo chini yake na lengo kubwa ni kupata na kutunza orodha ya wahitimu pamoja na anuani zao, kuandaa mikutano na makongamano yenye mada zinazohusu maendeleo ya chuo pamoja na serikali na jamii kwa ujumla na kutafuta vyanzo vya mapato ya kusaidia maendeleo ya chuo.


Katibu wa baraza hilo John Muruga alisema kamati yao imebaini kuwa udahili wa wanafunzi umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka 2016/ 2017 ni wanafunzi 2363 walidailiwa wanafunzi 553 wakiwa wa programu ya Astashahada, wanafunzi 471 wa programu ya Stashahada na wanafunzi 1339 wakiwa ni wa programu ya shahada ya kwanza.


"Idadi hii ya udahili inajumuisha pia wanafunzi waliodahiliwa katika Tawi la chuo cha Zanzibar ambao ni 354 " alisema Muruga.


(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »