Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini hotuba mbali mbali kabla hajahutubia hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, mjini Arusha.
Rais wa Mahakama ya Afrika Mhe. Jaji Justice Sylvain Ore akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
Wajumbe wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
Wajumbe wakipewa jarida la Mahakama ya Afrika mara baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada kuhutubia Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
……………………………………………………………..
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema
Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika kulinda na kutetea haki
za binadamu kwa kuzingatia maazimio mbalimbali ya ndani ya nchi na ya
kimataifa ikiwemo haki ya kuishi.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Arusha kwa niaba
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
wakati anafungua mkutano wa mazungumzo wa masuala ya demokrasia na haki
za binadamu ya Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za binadamu.
Amesema
Tanzania ni mfano wa kuigwa barani Afrika kwa kuzingatia na kutekeleza
ipasavyo mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolenga kuhakikisha
wananchi wake wanapata huduma bora na za msingi ikiwemo huduma ya afya
na elimu bila kubaguliwa kutokana na ulemavu,jinsia,rangi au dini.
Amesisitiza
kuwa Serikali itaendelea kutekeleza na kuzingatia matamko mbalimbali ya
Dunia yanayolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii
ikiwemo haki ya kuishi.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kufurahishwa na hatua
zinazochukuliwa na baadhi ya nchi za Afrika katika kulinda na kutetea
haki za binadamu hasa haki za wanawake na kusema kuwa bado kuna umuhimu
mkubwa kwa nchi ambazo zinazosuasua kutekeleza mikataba hiyo kufanya
hivyo ili kuhakikisha wanawake na watoto wanapata haki sawa katika
jamii.
Katika
hatua nyingine, Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali ya Tanzania
imepiga hatua kubwa katika kuingiza wanawake katika ngazi za maamuzi na
kwa sasa mpango kabambe unafanyiwa kazi ili kuhakikisha sekta binafsi
ambayo bado inaidadi ndogo ya wanawake kwenye ngazi za maamuzi kufanya
hivyo na kwamba tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini zinaonyesha kuwa
wanawake wengi walioingizwa kwenye bodi mbalimbali bodi hizo kwa sasa
zimeongeza ufanisi wa kazi maradufu.
Kwa
upande wake, Rais wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu
Justice Sylvain Ore amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwani unalenga
kujadili na kuweka mikakati inayolenga kuhakikisha nchi za Afrika
zinazingatia na kulinda haki za bindamu hasa haki za wanawake kwa
kiwango kikubwa.
Mkutano
huo wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu ambao unafanyika
Jijini Arusha umehudhuriwa na wajumbe kutoka mataifa mbalimbali ya
Afrika wakiwemo wajumbe kutoka Umoja wa Afrika AU na lengo la mkutano
huo ni kutajadili masuala ya demokrasia na haki za binadamu katika nchi
za Afrika.
EmoticonEmoticon