Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
Mdhibiti
na Mkaguzi mkuu wa Serikali (CAG),Profesa Mussa Assad ,amesema kuwa kwa
kipindi cha miaka kumi hadi kumi na tano iliyopita hapa nchini
watanzania wengi wamekuwa waongo, hali iliyochangia kuongeza kwa ukosefu
wa maadili.
Profesa
Assad ameyasema hayo alipokuwa anafunga mkutano wa wandishi wa habari
juu ya masuala ya maadhimisho ya siku ya maadili na utawala bora
yatakayofanyika Desemba 10 mwaka huu.
“Ndani
ya miaka 10 hadi 15 sasa,Watanzania wengi wamekuwa waongo sana kiasi
cha kupoteza maadili na uaminifu kwani swala hili la uongo limeshamiiri
sana katika matumizi ya simu kiasi cha kuathiri utendaji wetu wa kawaida
katika kazi za kila siku”amesema Profesa Assad.
Amesema
kuwa hata vyombo vingi vya habari hivi sasa vimeingia katika mpango huo
wa kuongopa kwa kushindwa kuandika habri za kina na zilizofanyiwa
utafiti ambao unatoa ushahidi wa moja kwa moja kwa jambo linalo andikwa.
Amemaliza
kwa kusema kuwa ni vyema watu wakaanza kupunguza uongo kwenye simu na
Maisha yao ya kila siku hili kuishi Maisha halisi yatakayowezesha
kupunguza uovu
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akitoa
utambulisho kwa Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na
Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya
Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji,
Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini Bw. Valentino
Mlowola akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi
na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (katikati) wakati wa uzinduzi wa
Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu,
Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo
jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali Prof. Mussa Assad.
Mgeni
Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.
Angellah Kairuki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili,
Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa
mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni
Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.
Angellah Kairuki (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini Bw. Valentino Mlowola
taarifa ya utekelezaji wa kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza
Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi
ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad na kulia ni
Mwenyekiti wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Bahama
Nyanduga.
Mwenyekiti
wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Bahama Nyanduga. akitoa
neno la shukrani kwa Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi
na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya
Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji,
Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema hii leo jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini Bw. Valentino
Mlowola (kulia) akijibu swali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili,
Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa
mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki na kushoto ni
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki
akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji
ya maadhimisho ya siku ya maadili kitaifa mara baada ya Mheshiwa Waziri
kuzindua rasmi Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za
Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa mapema
hii leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo.
EmoticonEmoticon