DC MTATURU: IKUNGI MARATHON KUFANYIKA KILA MWAKA

October 29, 2016

 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kulia akisistiza jambo wakati akizungumza na washiriki wa Ikungi Half Marathon kulia kwake ni MathiasCanal Mwandishi wa Habari wa mtandao wa Www.wazo-huru.blogspot.com
Afisa Michezo Wilaya ya Ikungi Aboubakary Kisuda akizungumza na awashiriki wa Ikungi Half Marathon kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Washiriki wa Ikungi Half Marathon wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu

 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu

Na Mathias Canal, Singida 

Mashindano ya kuibua vipaji vya wafukuza upepo kwa mbio ndefu Ikungi Half Marathon yanayotaraji kufika ukomo jumamosi hii Octoba 29, 2016 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika mashindano hayo.

Vijana takribani 60 shupavu waliochomoza kwenye mchujo wa ngazi ya Vijiji, Kata na Tarafa  wataingia barabarani kuisaka ama heshima ya ushindi au ushiriki kwa ngazi ya Wilaya huku wengine waliokosa nafasi katika awamu hii kusubiri awamu ijayo katika mashindano ya Full Marathon yatakayofanyika Mwaka 2017.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amezungumza na washiriki wote wa mbio hizo ambapo amewapongeza kwa kujitokeza kwa wingi jambo ambalo linaonyesha kuwa mchezo huo una wahitaji wengi.

Mtaturu amesema kuwa mashindano haya ya Ikungi Half Marathon yanafanyika kwa mara ya kwanza na yatakuwa endelevu ambapo mwakani yatafanyika pia mashindano yam bio ndefu yatakayojulikana kama Ikungi Marathon 2017.

Dc Mtaturu alisema kuwa Dhamira ya kuanzishwa kwa mashindano haya ni kuibua vipaji kwa vijana na kuviendeleza, Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa vijana na kuwaandaa vijana katika Wilaya hii kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

Mashindano ya mbio ndefu yenye umbali wa kilomita 21 yatahusisha vijana wenye umri wa kuanzia miaka 17 hadi 30 waishio Wilayani Ikungi na yanatarajiwa kufanyika kila mwaka ili kuinua hamasa ya Mchezo wa riadha huku yakiambatana na mbio fupi za mita 100, mita 400 na mita 800.

Mashindano haya yalianza Septemba 3, 2016 kwa ngazi ya Vijiji, Octoba Mosi yalifanyika kwa ngazi ya Kata, ambapo mchujo wa ngazi ya Tarafa imemalizika Octoba 15, 2016 na hatimaye kupisha mchuano wa Kiwilaya.

Mashindano haya yatatoa fursa kwa vijana kuonyesha uwezo wao wa kucheza na miguu kwa kasi ya ushindani kwa maana ya manufaa ya pesa lakini pia itaimarisha ajira kupitia chama cha Riadha mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla lakini pia kuwaondoa vijana wengi katika mawazo ovu ya kushinda vijiweni badala yake kujitokeza kwa ajili ya kujihusisha na Kilimo pamoja na ufugaji.
Dc Mtaturu amewasihi washiriki wote kukimbia kwa kutumia muda mzuri ili iwe taswira ya rekodi nzuri katika ukimbiaji jambo litakalokifanya chama cha cha Riadha Taifa kuchagua vipaji vitakavyoendelezwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »