Katikati Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Kushoto Mkuu wa
Wilaya ya Shinyanga Bi Josephine Matiru, na Bwana Daniel Sagata Pamoja
wakijiandaa kuanza zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Binzatana
Mjini Shinyanga mapema leo.
Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe Luahaga Mpina akishiriki katika zoezi la
kupanda miti Mjini Shinyanga leo.
Viongozi pamoja na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga katka zoezi la usafi wa mazingira mjini Shinyanga leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiongea na baadhi ya
wananchi wa mkoa wa Shinyaga katika eneo la Binzanata baada ya
kukamilisha zoezi la usafi wa mazingira na kupanda miti mapema leo.
Baadhi ya wakazi wa Mji wa Shinyanga wakishiriki katika zoezi la usafi wa mazingira leo, Mjini Shinyanga.
………………………………………..
EVELYN MKOKOI SHINYANGA
Uongozi wa mkoa wa Shinyanga
kupitia Mkuu wa Wilaya yake Bi Josephine Matiru umeiomba serikali
kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Kujenga kiwanda kitakacho tengeneza mkaa
utokanao na mabaki ya miti ambao ni rafiki kwa mazingira ili kunusuru
hali ya mkoa huo kuendelea kuwa jangwa kutokana na ukataji miti ovyo kwa
matumizi ya makaa manyumbani, matumizi mengine na athari zitokanazo na
mabadiliko ya tabia nchi.
Mkuu wa wilaya hiyo ametoa ombi
hilo leo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina aliposhiriki siku ya usafi kitaifa ya mwisho
wa mwezi October ambapo zoezi hilo lilizinduliwa rasmi na Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania December Mwaka jana na kuendelea
kutekelezwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kama siku maalum ya usafi
nchini.
Bi Materu aliendelea kusema kuwa,
Mkoa wa shinyanga unakumbana na changamoto kubwa ya ukataji miti ovyo
ambayo ingeweza kukabiliwa kwa kutumia mabaki ya miti, taka na maranda
ya mbao kutengeneza mkaa rafiki kwa mazingira na kusema kuwa mkoa na
wilaya ya shinyanga imebarikiwa kuwa na miti ya aina mbali mbali ambazo
mazingira yangetunzwa vizuri na kutumia malighafi hiyo ya taka
kutengeneza mkaa banifu akitolea mfano kiwanda cha kutengeneza mkaa
rafiki wa mazingira cha Zanzibar.
Kwa Upande wake Naibu Waziri Mpina
alikiri kupokea maombi ya mkuu wa wilaya huyo na kueleza kuwa serikali
itakuwa tayari kujenga kiwanda cha kutengeneza mkaa mjini shinyanga “Na
pengine katika Mbio za Mwenge Mwakani tukijaaliwa tunaweza kuzindua
kiwanda hicho kama mradi wa mfano.” Alisisitiza Mpina. “Lazima tuwe na
viwanda vya mkaa rafiki kwa mazingira sasa na wafanya biashara wa gas za
manyumbani sasa ufike wakati nao washushe bei ili asilimia kubwa ya
watanzania waweze kutumia nishati hiyo.” Alifafanua Mpina.
Akizungumzia suala ya usafi wa
Mazingira ambapo sambaba na hilo Naibu Waziri Mpina Pia alishiriki zoezi
la upandaji miti katika eneoa la Binzamata, alisema kuwa watanzania
wana kila sababu ya kujijengea utamaduni wa usafi wao pamoja na
mazingira kwani hata vitabu vitakatifu vinasisitiza usafi wa mazingira
akitolea mfano kitabu cha Biblia takatifu cha kumbu kumbu la Torati
23:11-14 na kusema kuwa “Pahala Pachafu hapana Utukufu wa Mungu na
hauwezi kuonekana mahali hapo na haya siyo maneno yangu wala ya Rais
Magufuli, ni maneno ya biblia hivyo watendaji katika ngazi zote
mzingatie utekelezaji wa sheria yya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni
zake na kuwachulia hatua wale wote watakao kiuka sheria hiyo.”
“Ni jukumu la kila mtu kufAnya
usafi na kila wilaya na Halmashauri ijetengenezee mwongozo na sheria
ndogo ndogo katika eneo hili la usafi wa mazingira na lazima watu
wawajibike.”
Naibu Waziri Mpina Pia alisisitiza
zoezi la upandaji miti ili kuweza kukabiliana na athari zitokanazo na
Mabadiliko ya tabia nchi na kurudisha uoto wa asili.
Akitolea mfano wa kasi ya serikali
ya awamu ya tano katika zoezi la usafi wa mazingira Mpina alisema “
watu walidhani Mhe. Rais alivyozindua siku ya usafi zilikuwa ni nguvu za
soda, kasi tuliyonza nayo ndiyo tutakayo maliza nayo, waharibifu wa
mazingira lazima sheria iwashughulikie.” Alisisitiza Mpina.
Akizungumzia wananchi wanaoabudu
siku ya Jumamosi Mpina alisema Sheria ndogo ndogo za mazingira za
Halmashauri na miji ni vizuri zikaona namna ya kuweza kuwapa nafasi na
wao ya kuabudu na kushiriki usafi katika siku hiyo.
Siku ya kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi imetengwa na serikali ikiwa ni maalum kwa ajili ya usafi nchini.
EmoticonEmoticon