Mhandisi wa Wakala wa barabara
Mkoa wa Mkoa John Kalupale (kwanza kulia) akiwatambulisha wawakilishi wa
Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd walipokuja kukabidhi msaada
wa mabati na Cement kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Maneja Mradi wa Kampuni ya
Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, Bw.Xie (kulia mbele) akimkabidhi Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (mbele kushoto) mfuko wa saruji na bati
kama sehemu ya msaada wa bati 500 na mifuko ya saruji 500 waliyoitoa kwa
ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za Maendeleo katika Mkoa wa
Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Mashaka Gambo (mbele) akishukuru Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture
Ltd kwa kutoa msaada kwa wananchi wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Mashaka Gambo(mbele kushoto) akikabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha mifuko
ya saruji 100 na bati 100 kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Muriet.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa
Arusha kupitia Tiket ya Ccm Catherine Magige(kwanza kushoto) akitoa
shukrani kwa kampuni ya Ujenzi iliyotoa msaada kwa ajili ya kuwezesha
huduma za kijamii Mkoani Arusha.
Mbunge wa Viti Maalum
anayewakilisha Kundi la Walemavu kupitia Tiket ya Ccm Amina
Mollel(kwanza kushoto) pia alitoa shukrani zake kwa kwa Kampuni iliyotoa
msaada.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha
Athumani Kihamia (pili kulia) akishkuru kwa msaada wa Mabati 100 na
Mifuko ya saruji 100 aliyopewa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya
Terrat.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo(kwanza kushoto) akimshkuru Meneja wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu
Joint Venture Ltd, baada ya kuhakiki msaada wa mabati 500 na mifuko ya
saruji 500.
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti
Maalum Amina Mollel, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro
pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Mhe. Catherine Magige baada ya
makabidhiano ya msaada wa mabati 500 na mifuko ya saruji 500 toka
kampuni ya ujenzi wa barabara ya Sakina Tengeru na barabara ya Mchepuko.
…………………………………………….
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo amepokea msaada wa bati 500 pamoja na mifuko ya saruji 500 kwa
ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa
zahanati pamoja na shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Arusha.
Mara baada ya kukabidhi wa msaada huo nje ya jengo la Ofisi
ya Mkuu huyo, Gambo alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel
Dararro mifuko 100 ya saruji na mabati 100 kwa ajili ya ujenzi kituo
cha afya kinachojengwa eneo la kwa mama mbauda kata ya Muriet Jijini
Arusha.
Alisema msaada huo utawezesha kila wilaya kunufaika nao
kwani kila wilaya za mkoa wa Arusha kuna changamoto za uhaba wa vyumba
vya madarasa pamoja na mahitaji ya majengo ya zahanati ili kusogeza
huduma kwa wananchi.
Alimshukuru Meneja Mradi wa Kampuni ya ujenzi ya Hanil –
Jiangsu Joint Venture Ltd, inayojenga barabara ya Sakina – Tengeru Km
14.1 na barabara ya Mchepuko Km 42.4 , Xie Jianbao ambao wametoa msaada
huo kama sehemu ya kurudhisha kwa jamii ya watanzania ili kukuza
mahusiano na kujali jamii na Taifa ambalo limewapa kazi kubwa ya ujenzi
wa barabar hiyo itakayogharimu takribani Bil. 139.
“Naishukuru kampuni hii kwa kutoa msaada huo kwa ajili ya
kuleta maendeleo na naahidi tutautumia ipasavyo katika kuleta maendeleo
na kila wilaya nitakayofanya ziara msaada huo nitaupeleka ili ya
kupunguza changamoto mbalimbali kwa jamii “.
Naye Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Bw. Xie alisema kampuni
yao imeona umuhimu wa kuchangia jamii kwani wao ni wajenzi wa barabara
na wanastahili kurejesha faida kwa jamii inayowazunguka.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro
alimshukuru Gambo kwa msaada huo na kusisitiza kuwa mifuko hiyo 100 ya
saruji pamoja na bati 100 zitasaidia ujenzi wa kituo cha afya
kinachojengwa Kata ya Muriet Jijini Arusha.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alishukuru
kwa msaada huo utakaosaidia ujenzi wa kituo cha afya kujengwa na
kukamilika ndani ya miezi miwili na kuahidi kwamba atasimamia ipasavyo
ili kuhakikisha Kituo kinajengwa katia ubora unaostahili.
Katika makabidhiano hayo
yaliyohudhuriwa na wabunge wa Viti maalum wanawake Mkoa wa Arusha,
Catherine Magige na Aminah Mollel walitoa rai kwa nyakati tofauti kwa
wananchi wa mkoa wa Arusha kumuunga mkono Mhe. Gambo pamoja na Serikali
ili kuwezesha maendeleo kusonga mbele.
EmoticonEmoticon