Uharibifu
wa Mazingira unaofanywa na binadamu, pichani ni Mto Kalembo uliopo katika
Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje uliochepushwa kwa manufaa ya baadhi ya
mtu/watu, haikuweza kufahamika mara moja muhusika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amemuagiza Mkuu wa wilaya ya
Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kutafuta wahusika na kuwafikishwa kwenye Vyombo
vya dola.
Na Lulu Mussa,Songwe
Wakazi
wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wamehamasishwa kutunza Vyanzo vya Maji kwakuwa
Maji hayana mmadala wa kitu chochote. Waziri wa Nchi mwenye dhamana ya
Usimamizi wa Masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameyasema
hayo leo katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua mazingira nchini.
Akiwa
katika Kijiji
cha Ibungu Wilayani Ileje, Waziri Makamba alishuhudia uliochepushwaji wa Mto
Kalembo kwa manufaa ya baadhi ya mtu/watu, na haikuweza kufahamika mara moja
muhusika. Aidha Waziri Makamba amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bw. Joseph
Modest Mkude kuhakisha wanambaini mtu/watu hao na kuwafisha katika vyombo vya
Sheria.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya
ya Ileje ilisema kwamba kumekuwa na uvamizi katika Vyanzo vya Maji na
Serikikali imeendelea na juhudi za kuwaondoa kwa kuwapatia maeneo mengine ila
baadhi ya wananchi hao wamekuwa wakikaidi. Hali hiyo haikumfurahisha Waziri
Makamba na kuagizia kutumika mamlaka ya Dola. "Hatuwezi kuruhusu watu
kuharibu Vyanzo vya Maji na kuwabembeleza watoke" Makamba alilisitiza.
Waziri Makamba amesema ni muhimu watu
kutii Sheria na Mamlaka zilizopo, ameagiza wakazi hao kupewa wiki mbili tu na
baada ya hapo waondolewe kwa nguvu kwani tayari maeneo mbadala kwa makazi yao
yalisha ainishwa. Pia Waziri Makamba ameahidi kutoa muongozo wa Sheria
ndogondogo za Mazingira za Vijiji na Vitongoji ili zitumike kama nyenzo za
hifadhi ya Mazingira Nchini.
Katika hatua nyingine Waziri Makamba
alitembelea Kijiji cha Lubanda, Kata ya Lubanda na kufanya Mkutano wa hadhara
na wananchi na kuwasisitizia, kutokokata miti ovyo, kutochoma misitu na kuepuka
uchepushaji wa Vyanzo vya Maji ikiwemo mito na Mabonde.
Pia Waziri Makamba aliwashauri wakazi
wa Lubanda kulima kilimo cha Matuta ama makinga maji ili kuepuka mmomonyoko wa udongo
katika miinuko. Aidha Waziri Makamba ameunga mkono jitahada za wananchi wa Kata
hiyo za ujenzi wa Kituo cha afya kwa kuchangia bati Ishirini na nane (28). Waziri
Makamba anaendelea na ziara yake na leo amewasili katika Mkoa wa Rukwa.
EmoticonEmoticon