Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’,
Charles Boniface Mkwasa, ametangaza wachezaji 20 watakaounda kikosi
kitakachosafiri mwishoni mwa mwezi huu kwenda Nigeria kwa ajili ya
mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.
Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa
kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini
utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G
ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo
iliyojitoa katikati ya mashindano.
“Tanzania hatuwezi kupuumza mchezo huu, tumeuchukulia serious (kwa
umakini) kabisa kwa sababu tunacheza ugenini ambako matokeo mazuri
yanaweza kutusongesha mbele na kuingia ndani ya timu 99 bora katika
viwango vya FIFA,” amesema Mkwasa.
Katika kikosi chake, Mkwasa ametangaza kutomjumuisha Mshambuliaji wa
Kimataifa, Thomas Ulimwengu anayecheza klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na majeruhi ya paja kama ilivyo
kwa Juma Abdul wa Young Africans ambaye aliumia katika mchezo wa kuwania
Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.
“Timu itaingia kambini Agosti 28, itakaa kambini kwa siku tano kabla
ya kusafiri kucheza mchezo huo wa kukamilisha ratiba ambao Misri tayari
wameshafuzu fainali za Afrika,” amesema Mkwasa na kuongeza kuwa kuna
mchezaji wa Tanzania, Said Carte Mhando anamfuatilia ili ikiwezekana
baadaye amwite kuchezea timu ya taifa. Anakipiga Klabu ya Brencia Calcio
ya Italia.
Wachezaji walioitwa:
Makipa-
Deogratius Munishi – Young Africans
Aishi Manula – Azam FC
Mabeki
Kelvin Yondani - Young Africans
Vicent Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji - Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe - Azam FC
David Mwantika - Azam FC
Viungo
Himid Mao - Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi - Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania
Washambuliaji
Simon Msuva - Young Africans
Jamal Mnyate – Simba SC
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco - Azam FC
Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji
EmoticonEmoticon