Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bwiru Mkoani Mwanza wakiwa wamekalia madawati 60 waliyopewa na kampuni ya Tigo,wakati wa hafla iliyofanyika jana. |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela(wa tatu kulia) akimpa mkono Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya,kwenye hafla ya kukabidhi madawati 60 kwa Shule ya Msingi Bwiru jana. |
•Shule 9 za msingi Mwanza zapokea madawati 385
Mwanza, Agosti 19, 2016: Kampuni ya Simu ya Tigo Tanzania leo imeanzisha rasmi mkakati wake wa nchi nzima wa kutoa huduma kwa jamii kwa kuchangia madawati 385 yenye thamani ya shilingi milioni 64 kwa shule tisa za msingi mkoani Mwanza ambayo yatazinufaisha shule za msingi katika wilaya za Ukerewe, Nyamagana, Ilemela na Sengerema wakati wa msimu wa tamasha la Fiesta 2016 mkoani Mwanza
Kukabidhiwa kwa madawati hayo mkoani Mwanza ni matokeo ya juhudi zinazoendelea za Tigo za kuwekezaq katika elimu na hususani katika kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi za umma nchi ambapo mikoa 18 itanufaika katika msimu wa Fiesta 2016. Ikumbukwe kwamba kwa mwaka huu kampuni imeshachangia madawati 5,700 kote nchini na hivyo kuwa imewakalisha wanafunzi 17,000 ambao awali walikuwa wakikaa sakafuni.
Mkakati wa kutoa msaada wa madawati katika msimo huu wa Fiesta unajulikana, “‘Dawati kwa kila mwanafunzi ni msingi wa elimu bora; Fiesta 2016 kwa Kishindo cha Tigo Elimu bora, Imooooo!’
Akizungumza katika sherehe za kukabidhi madawati hayo zilizofanyika katika Shule ya Msingi Bwiru Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ally Maswanya, alisema uhaba wa madawati katika shule za msingi unajulikana kama moja ya sababu zinazoathiri kujifunza pamoja na ufanisi wa wanafunzi katika shule zetu nyingi za msingi.
“Tumejikita katika kuhakikisha kuwa mazingira ya kujifunzia katika shule zetu za msingi yanaboreshwa na tunayofuraha kwamba Tigo inabadilisha kizazi cha baadaye am,bacho ni wanafunzi katika shule za msingi kwa kuhakikisha hawakai chini tena. Tunaamini kwamba msaada huu utaenda mbali katika kuwasadia wanafunzi kuzifikia ndooto zao za kuwa viongozi wa baadaye kutokana na kuondoka kwa bughudha na hivyo kujikita katika masomo,” alisema Maswanya.
Makabidhiano ya madawati hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela ambaye alisema kuwa madawati 385 yataboresha kwa kiwango kikubwa mazingira ya kujifunza kwa watoto katika mkoa huo na kuwataka watu wengine wenye mapenzi mema kujitokeza na kujiunga na juhudi hizo za kuondoa uhaba wa madawati uliobakia katika mkoa huo.
Mongela alizitaja shule zitakazopokea madawati hayo na idadi katika mabano kuwa ni Nakoza (29), Uhuru (40), Busangu (41), Bukongo (30), Nansio (30), Namagubho (30), Mkuyuni (65) Chambanda (60) na Bwiru (60) .
“Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa kutuunga mkono katika juhudi zetu kwa kupunguza kiasi cha uhaba wa madawati katika shule za msingi mkoani Mwanza. Tunaamini madawati haya 385 yatatufikisha mbali katika kuwawezesha mamia ya watoto kuwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia yanayotakiwa kwa ajili ya mafanikio katika elimu yao,” alisema Mongela.
EmoticonEmoticon