Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akisisitiza jambo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari kutoka katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Sunshine Muslim
Volunteer huku wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi za Uingereza,
Afrika kusini, Canada na Pakistani waliokuja kuweka kambi ya siku tano kwa
ajili ya kutoa matibabu bure ya Fistula.
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF), Mussa Mbaruku ameombwa kuangalia namna ya
kuweka mkakati wa kuvisaidia vituo vya afya na Zahanati zilivyopo ndani ya Jiji
la Tanga ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya mkoa wa Tanga
Bombo inayohudumia wagonjwa wa mkoa mzima.
Ombi hilo lilitolewa jana na Mganga Mku wa Mkoa wa Tanga (RMO) Asha Mahita
wakati Mbunge huyo alipoitembelea hospitali ya alisema kuwa msongamano
unaoikabili Hospitali ya Rufaa ya Mkoa unatokana na kutokuwepo na ubora katika
zahanati na vituo vya afya jambo ambalo linalowafanya wanachi kukimbilia katika
Hosptiali hiyo.
Hatua hiyo inatokana na zahanati na vituo vya afya vingi Jijini Tanga kukakabiliwa
na changamito nyingi zinazo sababisha kukosa ubora hali inayochangia kwa
asilimia kubwa wananchi wengi kukimbilia katika hospital ya Rufaa ya Bombo na
kuongeza msongamano wa wagonjwa.
Mahita alisema ipo haja ya kuvisaidia vituo hivyo ambavyo havina nyumba za
watumishi, uzio, miundombinu mibovu na vingine kukosa umeme jambo ambalo
linakuwa si rafiki kwa wahudumu na linakwamisha shughuli za kiafya hasa nyakati
za usiku.
Alisema kuwa iwapo kutakuwepo na mabororesho katika vituo hivyo huku Serikali
na wadau mbalimbali wakiweka nguvu zao katika swala la kumalizia Hospitali ya wilaya
ambayo mpaka sasa inajengo moja la ghorofa kwa ajili ya utawala ikimaliziwa na
kuanza kutumika kutapunguza kwa asilimia kubwa msongamano kwenye hospitali hiyo.
Kwa upande wake, Mbunge Mussa Mbaruku alihaidia kuangalia namna ya kuzipatia
ufumbuzi changamoto hizo kwani wananchi afya zao zinapokuwa zimeimarika
inawasaidia kuweza kufanya shughuli za kujiingizia kipato.
“Ndugu zangu huu si muda wa kupiga porojo kuhusiana na masuala ya afya
ambalo ndio uti wa mgongo wa wananchi hivyo lazima viongozi wajenge umoja na kutafuta njia
ya kuweza kuviboresha vituo hivyo ambavyo vitawasaidia kwa asilimia kubwa
wananchi kupata huduma hiyo kwa ukaribu zaidi “Alisema
Aidha alisema pamoja na changamoto zinazozikabili zahanati na vituo hivyo
lazima Serikali itenge fedha za kutosha ili kuweza kuimalizia Hospitali ya
Wilaya iliyopo Masiwani Shamba ambayo mpaka sasa bado hakuna majibu sahihi ya
kukwama kwa umaliziwaji wa Hosptili hiyo.
“Bado nashindwa kupa majibu ni kitu gani kinachokwamisha kumalizika kwa
Hospitali ya Wilaya ambayo tayari inajengo zuri la utawala tena la ghorofa
serikali inawajibu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Hospitali
hiyo inamalizika na inakuwa na kiwango bora katika sekta zote za matibabu.
Mbaruku alifanya mazungumzo hayo na mganga mkuu wa Mkoa alipo watembelea
madaktari kutoka katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Sunshine Muslim
Volunteer huku wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi za Uingereza,
Afrika kusini, Canada na Pakistani waliokuja kuweka kambi ya siku tano kwa
ajili ya kutoa matibabu bure ya Fistula.
EmoticonEmoticon