Mchezo Mpira wa Miguu wa Ufukweni kati ya Tanzania na Ivory Coast
kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa utachezeshwa na
waamuzi kutoka Uganda ambao ni Shafic Mugerwa katikati na wasaidizi wake
ni Ivan Bayige Kintu na Muhammad Ssenteza.
Mtunza muda katika mchezo huo atakuwa Adil Ouchker wa Morocco huku
Kamishna akiwa ni Reverien Ndikuriyo wa Burundi. Timu hizo zinatarajiwa
kucheza mechi mbili ambako mara baada ya mchezo wa Dar es Salaam,
utarudiwa mwingine huko Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa
amefanikiwa kufuzu kwa fainali.
Kocha wa timu hiyo, John Mwansasu, leo Agosti 12, 2016 ametangaza
kikosi cha wachezaji 16 watakaoingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na
mchezo huo utakaofanyika Agosti 26, mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari Mwansasu amesema kikosi hicho kinaundwa na wachezaji sita kutoka Zanzibar na 10 Tanzania Bara.
Pia Mwansasu amesema wanatarajiwa kucheza mechi mbili ambako mara
baada ya mchezo wa Dar es Salaam, watarudiana huko Ivory Coast na
mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.
Kikosi hicho kinaunda na wachezaji Talib Ame,
Ahamada, Mohammed Makame, Ahamed Rajab (golikipa) Khamis Said na Yacob
Mohamed wote kutoka Zanzibar.
Wengine ni Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland
Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma
Juma na Kevin Baraka.
EmoticonEmoticon