OFISI YA MAKAMU WA RAIS
ZANZIBAR
Wakazi wa kijiji cha Kizimkazi
kilichopo katika jimbo la Makunduchi Mkoa
wa kusini unguja, kimekuwa na utaratibu wa kuadhimisha siku ya kizimkazi,
maarufu kama kizimkazi day ambayo
hufanyika kila mwaka mwezi wa nane.
Siku hiyo maarufu katika kijiji hicho
ambayo imeanzishwa na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo la Makunduchi
mhe.Samia Suluhu Hassan ambae sasa ni Makamu wa Rais wa JAmuhuri ya muungano wa
Tanzania imekuwa ikiadhimishwa kijijini hapo kwa namna ya kipekee ya burudani,
mashairi na michezo mbali mbali ambapo pia wana kizimkazi wamekuwa wakipata
nafasi ya kuainisha changamoto mbali mbali zinazo wakabili kagtika kijiji
hicho.
Akimuwalisha Makamu wa Rais Mhe.
Samia Suluhu Hassan, Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa RAis Muungano na Mazingira
Mhe Luhaga Mpina amehaidi kutatua baadhi ya changamoto mbalimbali
zinazowakabili wakazi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la
Makunduchi mhe. Haruna Suleiman ambae pia ni Waziri wa Katiba, Sheria Utumishi
wa Umma na Utawala bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuchangia
mifuko 100 ya simenti na mabati 100, na matofali 2000 ya kuanza ujenzi wa
vyumba vya madarasa ambavyo vimeanishwa kuwa moja ya changamoto kijijini hapo.
Aidha, amehaidi wana kizimkazi kuwa
kwa kushirikiana na mbunge na uongozi wa serikali uwanja wa mpira ambao umekuwa
ukihitaji matengezo nao utaanza kusawazishwa kwa ajili ya michezo kijijini
hapo.
Wana Kizimkazi wamebainisha
kukabiliana na changamoto itokanayo na mapato na matumizi ya rasilimali ya
bahari, pamoja na kupungua kwa nishati ya umeme kutokana na ongezeko la
mahitaji litokanalo na mji huo kupanuka.
Kwa upande mwingine Naibu Waziri
Mpina Pia alimuwailisha Makamo wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika
kampuni inayotengeneza nishati ya mkaa rafiki wa mazingira inayotumia malighafi
itoknayo na taka za maganda ya miwa na
makarati na kuwapongeza kwa jitihada kubwa za utunzaji wa mazingira kwa
kutokukata miti ovyo na ubunifu wa nishati hiyo.
Ziara ya naibu Waziri Mpina Mjini
Zanzibar ni Sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake katika Ofisi ya Makamu wa
Rais, Pamoja na kumuwakilisha Mhe, Makamu wa Rais katika siku maalum ya Kizimkazi.
Kizimkazi Day.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi
Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina aliyevaa suti akishika na kuangalia
nishati ya mkaa unaotengenezwa na
malighafi itokanayo na taka za miwa na karatasi mjini Unguja, alipomuwakilisha
Makamu wa Raisi Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kampuni ya Blue Spot,
inayotengeneza nishati hiyo bila kuharibu Mazingira.
Aliyesimama Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Pamoja na baadhi
yaViongozi mbali mbali wa jimbo la Makunduchi mkoa wa kusini Unguja,
akizungumza na wanachi (hawapo pichani) wa jimbo hilo katika kijiji cha
kizimkazi .katika siku ya kizimkazi maarufu kama kizimkazi day, alipomuwakilisha
mhe. Mkamu wa Rais Mama Samia Suhulu Hassan aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo
hilo.
Aliyesimama katikati Mkurugenzi wa Kampuni ya Blue Spot Bw Buhet Juma ya Mjini Unguja inayotengeneza nishati ya mkaa ambayo ni rafiki kwa mazingira akimuonyesha Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira aliyesimama kushoto, ambavyo nishati hiyo inavoengenezwa
Aliyekaa katikati Naibu Waziri Ofisi
ya Makamu wa Ris Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katika Picha ya Pamoja
na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Raisi, Pamoja na wafanyakazi wa
kampuni ya kutengeza nishati ya Mkaa rafiki wa mazingira, katika kiwanda cha
Blue Spot. (Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.)
EmoticonEmoticon