BOHARI LATEKETEA KWA MOTO SINZA LEGO JIJINI DAR JIONI HII

August 01, 2016
Bohari likiwa linateketea kwa moto jioni hii Sinza Lego
Mmoja wa kijana ambaye alifika kushuhudia tukio hilo akipanda juu ya Ghorofa baada ya kunusurika kudondokea katika moto huo
Moto ukiendelea kuwaka huku juhudi za kuzima zikiendelea
Mbele ni Gari la zima moto likiwa limefanya juhudi za kuzima moto ,  hapa wakiondoka kufuata maji mengine ili kuendelea na zoezi la kuzima moto huo
Moto ukiendelea kuwaka katika Bohari hilo
Baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia tukio hilo la kuwaka kwa Bohari
Magari yakiwa yameruhusiwa kuendelea na safari baada ya moto huo na moshi mkubwa kupungua 

Picha na Fredy Njeje/Blogs za mikoa
Bohari moja ambalo lilikuwa la kuhifadhia mataili pamoja na vifaa vyenginevyo vya magari lililopo Sinza Lego ambalo mmiriki wake hakufahamika kwa mara moja limeteketea kwa moto ambapo kwa mujibu ya wenyeji wa eneo hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo ni mataili.  Pia katika eneo hilo kuna Gereji ambayo haikuathirika na moto huo mkubwa, mpaka jioni hii kikosi cha kuzima moto kilikuwa eneo la tukio kuendelea kusaidiana na wananchi kuhakikisha moto huo unazimika. Taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi.
Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 Mob +255 654221465 E-Mail blogszamikoa@live.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.blogszamikoa.com 1458109219454_logo_blog_za_mikoi.png

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »