Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
(katikati) akiangalia samaki katika soko ya wilaya ya Masasi akiwa
katika ziara yake ya usafi na ukaguzi wa mazingira mjini Masasi, (kilia)
ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bw. Selemani Mzee.
Aliyeinama
katikati akikusanya uchafu ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akishiriki katika zoezi la usafi
wa mazingira Wilayani Masasi mwishoni mwa wiki.
Bw.
Benjamini Elias (kulia) Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Masasi
akitoa taarifa na maelezo ya hali ya usafi wa soko la mji wa Masasi kwa
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina
(kushoto), wakati wa ukaguzi wa usafi wa mazingira mjini Masasi.
(PICHA NA EVELYN MKOKOI)
……………………………………………………………………………………………
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) amezitaka
Radio za jamii kuhamasisha usafiri wa mazingira nchini. Naibu Waziri
Mpina ametoa kauli hiyo alipokuwa akishiriki siku ya usafi kitaifa,
mwishoni mwa wiki wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Akitolea Mfano wa Radio Pride FM
ya Mjini Mtwara yenye kupatikana katika frequencies 87.8 mjini Mtwara,
ambayo imeanzisha kampeni ya usafi katika mkoa wa mtwara na wilaya zake
kwa kufanya vipindi vya moja kwa moja na kutembelea wilaya za mkoa huo
kufanya usafi wa mazingira kwa vitendo.
Kwa Upande wake Bw. JUma Andrea
Manager uzalishaji wa kituo hicho cha Radio, alisema kuwa lengo kubwa la
kituo hicho kuhamasiha usafi ni kuunga mkono agizo la Mhe. Rais kwa
kuwaweka pamoja wananchi, kuweka muamko na hamasa ili kujenga tabia ya
kupenda usafi na kuepukana na magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea
mfano ugonjwa wa homa ya matumbo na kipindipindu.
Akiongea na Uongozi wa Mkoa wa
Mtwara katika majumuisho ya ziara yake Wilayani Masasi, Naibu Waziri
Mpina aliwataka viongozi wa mkoa huo kuunda sheria ndogondogo za
mazingira zitakazo watoza faini wananchi waharibifu wa mazingira mkoani
humo, na kuwachukulia hatua za kisheria kulingana na hali ya wananchi
ili waweze kujifunza na kujijengea tabia ya usafi.
“Nimeona kuwa uchomaji moto
misitu ovyo hapa kwenu umekithiri, uchomaji moto taka nao siyo njia
nzuri ya uondoshwaji wa taka,hiyo kuwe na miondombinu rafiki kwa
uondoshwaji wa taka, na kiongozi wa mkoa ambae hatakuwa tayari
kushughulikia usafi wa mazingira na yeye awe tayari kushughulikiwa
alisisitiza.”
Ziara ya Naibu Waziri Mpina
Mkoani Mtwara ni muendelezo wa Ziara zake nchini za ukaguzi wa viwanda
na usafi wa mazingira iliyohusisha pia ukaguzi wa machinjio ya mji wa
Masasi.
EmoticonEmoticon