Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kesho Jumamosi Julai
30, 2016 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mashindano ya
kuibua na kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu
ya Karume ulioko kwenye makutano ya Barabara za Uhuru na Shaurimoyo,
Ilala jijini Dar es Salaam.
Sambamba na Makonda, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi naye amethibitisha kuwako kwenye hafla hiyo ambayo
mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za Ilala Boys dhidi ya Bombom
Ilala, Dar es Salaam. Inawakilishwa na mikoa yote mitatu kisoka ambayo
ni Ilala, Kinondoni na Temeke kwa pande zote mbili za wavulana na
wasichana.
Kadhalika, wakuu wa mikoa mingine ambayo
mashindano hayo yatafanyika nao watakuwa wageni rasmi katika mikoa yao
ambayo ni Mbeya, Mwanza na Morogoro kwa upande wa wavulana pia Arusha,
Lindi na Zanzibar kwa upande wa wasichana.
EmoticonEmoticon