Makamu
wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza
na Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhan Feruzi
(katikati)
ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali
Ndugu Said Mohamed mkazi wa Mafia ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road, Mkazi huyo wa Mafia alimueleza Makamu wa Rais juu ya ugumu wa
upatikanaji wa Dawa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Bi.
Maria Maliseli Boniface wa Kilosa Morogoro ambaye amelazwa katika Taasisi ya
Saratani ya Ocean Road.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali
Ndugu Calist P. Mushi mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro ambaye amelazwa katika
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean
Road Dk. Diwani Msemo (kulia) wakati wa kutembelea Taasisi hiyo iliyopo
jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na
wananchi waliokuja kuwaona ndugu na jamaa zao ambao wamelazwa katika
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Wananchi hao walimueleza Makamu wa Rais haja
ya kuongezwa kwa mashine za mionzi suala ambalo Makamu wa Rais aliwajibu kuwa
zitafungwa mashine mpya mbili katika mwaka huu wa fedha 2016-2017
ilikurahisisha matibabu.
.............................. .....
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa
serikali itanunua mashine mbili za kisasa
za mionzi kwa ajili ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ambazo zitasaidia kwa
kiasi kikubwa utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kupata matibabu katika
Taasisi hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Sulu Hassan ametoa ahadi
hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara
fupi ya kutembelea Taasisi ya Saratani ya Ocean Road pamoja na Kumtembelea na
kumpa pole Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhani Feruzi ambaye
anapatiwa matibabu kwenye Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa mkakati uliopo wa serikali unalenga kuhakikisha kuwa
hali ya utoaji wa huduma za afya na dawa kote nchini unaimarika maradufu ili
wananchi waweze kupata huduma hizo kwenye maeneo yao kwa ubora unatakiwa.
Kuhusu
uhaba wa wahudumu wa afya katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ameuahidi uongozi wa Taasisi hiyo kuwa serikali
itahakikisha wahudumu hao wanapatikana katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Baadhi ya
wagonjwa na wananchi wamepongeza utoaji wa tiba katika Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road na wameomba serikali iendelee kuipatia taasisi hiyo vifaa vya kisasa
vya kutolea tiba kama hatua ya kuboresha utoaji wa matibabu kwa wagonjwa
wanaokwenda kupata matibabu ya saratani.
EmoticonEmoticon