Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano
na Mazingira Mh.Luhaga Mpina (Kulia) akifurahia Jambo na Meneja Mahusiano
wa kiwanda cha Pepsi bw,Alexander Nyirenda alipotembelea kiwanda hicho
kilichopo kiwalani Temeke Jijini Dar es salaaam mapema hii leo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano
na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiwa ameambatana na Maafisa wa Mazingira
kutoka Baraza la Usimamizi wa Mazingira Nchini( NEMC)akikagua mfereji
unaotiririsha maji machafu kutoka katika kiwanda hicho na kusababisha
madhara kwa wanainchi wanaozunguka eneo hilo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano
na Mazingira Mh,Luhaga Mpina akiongea na waandishi wa habari mara baada
ya kufanya ziara katika kiwanda cha pepsi kilichopo kiwalani,temeke
jijini dar es salaam
EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI OFISI YA MAKAMU WA RAIS
KIWALANI-DAR ES SALAAM
19/7/2016
Kiwanda cha kutengeneza kinywaji cha soda aina ya Pepsi kilichopo Kiwalani
jijini jijini Dar es Salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni 25
na kutakiwa kulipa faini hiyo ndani ya siku kumi na nne kwa kosa la
uchafuzi wa mazingira, kwa kutiririsha maji machafu yenye kemikali katika
mtaro wa maji ya mvua ya mtaa wa kiwalani.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limetoa
adhabu hiyo ya ukiukwaji wa sheria ya mazingira na kanuni zake ya mwaka
2004, kupitia ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ya kukagua mazingira ya jiji la Dar
es Salaam na mitaa ya viwanda.
Naibu Waziri Mpina alisema kuwa wawekezaji wenye viwanda wanapaswa
kuelewa kuwa NEMC huwa inapita mara kwa mara na kutoa mwongozo, wa utekelezaji
wa sheria ya mazingira na kuwataka wawekezaji waache dharau ya kuthaminisha
maisha ya wananchi kwa gharama ndogo, na kuwaasa wawe serious na sheria ya mazingira, na kuwaonya
wamiliki wa kiwanda cha SBC Tanzania Limited. kuacha kabisa kutiririsha
maji machafu, pamoja na kuelekeza kila kiwanda kiwe na Afisa Mazingira
ambae ndiyo mshauri mkuu wa masuala ya mazingira.
Aidha Mhe. Mpina aliwataka wawekezaji pia wapeleke kwake malalamiko
ya watendaji wa NEMC ambao wanaona hawawatendei haki.
Awali akitamka adhabu hiyo Mkaguzi Mkuu wa Kanda ya Mashariki
kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Bw.
Jaffari Chimgege alisema kuwa pamoja na adhabu hiyo kiwanda hicho
cha Pepsi pia kimekuwa na kosa la kutiririsha maji hayo machafu bila
kuyatibu na kwa mujibu wa sheria ya wenye viwanda walitakiwa kukusanya
taarifa ya ukaguzi kwa baraza, ili kuona kama wanatekeleza sheria ya
mazingira na hawakufanya hivyo.
“Wafanyie kazi haraka taarifa ya ukaguzi.”
Kwa upande wake, Afisa Mauhusiano wa kiwanda hicho Bw. Alexandra Nyirenda
aliliomba Baraza (NEMC) kuelekeza wenye viwanda zaidi ya mara mbili
kabla ya kutoa adhabu, ili waweze kwenda sawa na utekelezaji wa
Sheria ya mazingira na kanuni zake kwani kujisahau ni ubinadamu.
Wakati huo huo; Mhe Naibu Waziri Mpina amezindua bomba lenye urefu
wa kilometa mbili la, utoaji maji taka katika kiwanda cha bia cha Serengeti.
(SBL) cha Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.
EmoticonEmoticon