Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula
akipekua mafaili ya hukumu za migogoro ya ardhi ili kujiridhisha kama
haki inatendeka kwa wananchi wakati alipotembelea Baraza la Ardhi na
Nyumba la Tanga mjini.
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.
Baadhi
ya watendaji na watumishi wa umma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula katika ofisi za
Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.
…………………………………………………………………………………………………
Na Hassan I. Mabuye
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula
ayataka Mabaraza ya Ardhi na Nyumba kuepuka rushwa kutoka kwa wenye
fedha ili kuwapa upendeleo na kukandamiza wanyonge katika maamuzi
yahusuyo migogoro ya ardhi.
Mheshimiwa Mabula ameyasema hayo wakati
alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.
Wakati wa ziara hiyo Mhe. Naibu Waziri amepiga marufuku tabia ya baadhi
ya watu ambao huwapa pesa waendesha mashtaka na wenyeviti wa mabaraza
ya Ardhi na nyumba ili kupindisha sheria.
EmoticonEmoticon