Msajili
wa Hazina, Lawrence Mafuru (katikati), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu msimamo wa Serikali kuhusu
Benki ya Twiga Bancorp. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo,
Cosmas Kimario na Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala, Amina Lumuli.
Maofisa wa Benki hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Mpiga picha za magazeti Loveness Benard akiwa kazini ‘ hapana kuchezea kazi hapa kazi tu’
……………………………………………………………………
MSAJILI
wa Hazina Ndugu Lawrence Mafuru ametolea ufafanuzi taarifa iliyotolewa
na vyombo vya habari kuhusu msimamo wa Serikali kwa Benki ya
Twigabancorp.
Taarifa
hiyo ilieleweka vibaya kuhusu msimamo wa Serikali kwa benki hii ya
Twiga Bancorp. Naomba nieleze kwamba kwa hivi sasa Serikali inasubiri
mapendekezo ya kitaalamu yatakayowezesha kutatua changamoto za kimtaji
za Twiga Bancorp.
Ninaposema
changamoto za kimtaji sijasema kwamba benki hiyi ipo kwenye hali mbaya
ya kushindwa kujiendesha, ila inahitaji nyongeza ya mtaji kwa ajili ya
kutekeleza matakwa ya kisheria na vilevile kuimarisha na kusambaza
huduma mbalimbali katika maeneo ya nchi. Hatua hizo zinafuatia agizo la
Mheshimiwa Rais kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipangokufuatilia
utendaji wa benki ya Twiga Bancorp na kuhakikisha kasoro zilizopo
zinatatuliwa.
“Kuna
njia mbalilimbali za kuiwezesha benki kupata mtaji ikiwemo nje ya
utaratibu wa Serikali, ndiyo maanaWizara na Ofisi ya Msajili wa Hazina
ikishirikiana na Manejiment ya Twiga Bancorp zinaandaa mapendekezo
yatakayoiwezesha Benki hii kupata mtaji ili kuiwezeshakutimiza malengo
yake ya kiukuaji na kujiendesha kwa faida.”
Hatua
mbalimbali zilianza kuchukuliwa na Wizara ya Fedhana Mipango na ofisi
ya Msajili wa Hazina kwa ajili ya kuboresha utendaji wa Benki ya Twiga
Bancorp. Kwa mfano, mnamo mwaka 2015, Muundo wa Shirika ulibadilishwa
ambao pamoja na mambo mengine ulipelekea kuteuliwa kwa Menejimenti mpya,
kwa kupitia Menejimenti hiyo mpya umetengenezwa Mpango Mkakati wa
miaka mitano ambao umeanza kutumika Januari 2016, serikali pia ilifanya
mabadiliko katika bodi ya wakurugenzi kwa kuteuaBodi mpya ya
Wakurugenzi.
Kwa
ujumla kuna mabadiliko makubwa ya kiutendaji baada ya hatua hizo
kuchukuliwa. Kwa mfano benki imeweza kupata Hati Safi ya Mahesabu
(Unqualified Opinion) kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Heasabu za
Serikali kwa mara ya kwanza kwenye hesabu zake za mwaka 2015 jambo
ambalo halikuwezekana toka Mwaka 2011.
“Hizi
taarifa zinazosambaa kuwa benki inafungwa sio za kweli. Kwenye benki
kuna pesa za wananchi, kuna mikopo iliyotolewa kwa watu mbalimbali, kuna
rasilimali za benki ikiwemo rasilimmali watu. Yote hayo yana Utaratibu
wake wa kuyasimamia.. Hata ukisikiliza hotuba ya Rais hakusema funga
benki ya Twiga Bancorp aliagiza hatua zichukuliwe na kwamba Katibu Mkuu
asimamie.”
Hivyo
tuna wahakikishia kuwa fedha za wananchi zilizo katika benki ya Twiga
Bancorp zipo salama na kwamba uongozi uliopo hivi sasa unaendelea
kushughulikia changamoto za kiutendaji zilizokuwepo na kama yalivyokuwa
maagizo ya Rais hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa kwa ajili ya
kuhakikisha mambo yote yanakuwa sawa. Pia benki hii inaendelea kutoa
huduma zake kwa wateja kama kawaida.”
Mwisho,
Serikali itaendelea kutoa msukumo kwa benki hiiili kuhakikisha tatizo
lililopo sasa la mtaji linatatuliwa na kuhakikisha inajiendesha kwa
faida.
EmoticonEmoticon