Kaimu
Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya
Zanzibar, Dkt. Mahmoud Ibrahim Mussa akitoa mafunzo juu ya kuwasaidia
watumiaji wa madawa ya kulevya kwa Askari wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar
katika ukumbi wa Chuo hicho Kilimani Mjini Zanzibar.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya kuwasaidia watumiaji wa madawa ya kulevya
wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana
na Madawa ya Kulevya Zanzibar Dkt. Mahmoud Ibrahim (hayupo pichani)
katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika ukumbi wa Chuo hicho.
Picha na Haji Ramadhan Suweid.
Na Miza kona – Maelezo Zanzibar
Matumizi
ya dawa za kulevya ni janga linaloathiri vijana na kupoteza mwelekeo
ambao hupelekea kufanya maamuzi yasiyo sahihi na kupoteza kumbukumbu
jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya Taifa.
Akitoa
mafunzo kwa watendaji wa Chuo cha Mafunzo Kaimu Mkurugenzi Tume ya
Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Dkt Mahmoud Ibrahim
Mussa katika shamra shamra za kuadhimisha siku ya kudhibiti madawa ya
kulevya.
Amesema
mtumiaji wa madawa ya kulevya huathirika ubongo ambao hawezi kuacha
kutumia madawa hayo kwa kuongeza kiwango hali ambayo inayopelekea
kutoweza kufanya shughuli za kimaendeleo.
Ameeleza
kuwa maambukizi makubwa ya virusi vya ukimwi yanasababishwa zaidi na
watumiaji wa madaya ya kulevya kwa njia ya kujidunga sindano ambayo
yanaathiri jamii na kupoteza nguvu ya taifa.
“Sigara
ina madhara makubwa nacho pia ni kilevi ina kemikali 4000 ambayo
huleta madhara kwa binadamu na kuharibu viungo, husababisha maradhi ya
moyo, kansa pia hupelekea ugonjwa wa akili,” alitanabahisha Dkt
Mahamoud.
Amefahamisha
jamii itanabahishwe zaidi juu ya madhara ya matumizi dawa za kulevya
pamoja na uvutaji wa sigara jinsi ya kuyaepuka na na kuwasaidia
watumiaji wa madawa ya kulevya ili kuweza kuyaacha madawa hayo.
Dkt
Mahamoud amefahamisha kuwa kinga ya msingi ya kuachana matumizi ya dawa
za kulevya imo ndani ya familia ambayo iweze kumkubali muathirika ili
aweze kuachana na kilevi kwa kumpa huduma nzuri bila ya kunyanyapaa.
Aidha
wameshauri kutafuta njia ya kuweza kudhibiti utumiaji wa dawa za
kulevya katika Vyuo vya mafunzo kwa wafungwa kwani imebainika kuwa
baadhi yao hutumia dawa hizo wakati wanatumia kifungo.
Nao
washiriki wa mafunzo hayo wameiomba jamii kutoa mashiriakiano makubwa
na vyombo vya kudhibiti madawa ya kulevya ili kuweza kuwafichua na
kuwadhibiti wale wote wanaoingiza, wanaosambaza na watumiaji pamoja na
kutoa elimu hiyo kupitia skuli mbali mbali ili kuhakikisha kuwa jambo
hilo linadhibitiwa nchini.
Aidha
wameitaka Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya kuwa huru katika kutoa
huduma zake ii iweze kufanyakazi kwa uwazi pamoja na wazazi kuwafundisha
watoto wao maadili mema na kukua katika misingi mizuri kwani vishawishi
vya madhara hayo ni vijana.
Mafunzo
hayo ni ya siku moja ambayo yaliyowashirikisha watendaji wa Chuo cha
Mafunzo ambapo kilele chake kinatarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.
EmoticonEmoticon